Mbowe atembelea shamba lake alilopigwa marufuku asilime

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,808
20,223
Hai. Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ametembelea shamba lake la kilimo cha kisasa cha mboga mboga ( Green House) yaliyopo Hain na kuwajulia hali wafanyakazi pamoja na wataalam wake leo Ijumaa.

Pia, Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa nayo ya kupoteza ajira zao wanazozitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasiu Byakanwa kupiga marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe.

Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani shamba hilo lipo ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.




Chanzo: Mwananchi
 
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ametembelea shamba lake la kilimo cha kisasa cha mboga mboga ( Green House) yaliyopo Hain na kuwajulia hali wafanyakazi pamoja na wataalam wake leo Ijumaa.


Pia, Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa nayo ya kupoteza ajira zao wanazozitegemea katika kuendesha maisha yao yakila siku.


Hali hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, GellasiuByakanwa kupiga marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la Kilimanjaro Veggies linalomilikiwa na Mbowe.


Byakanwa alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilolenye ukubwa wa hekari mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani shamba hilo lipo ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.





Chanzo : Mwananchi Online
 
Kumbe ni Greenhouse? zinaharibu chanzo cha maji kivipi, maana zinatumia maji kiasi kidogo sana, kutokana na kutokuwepo kwa evaporation
Waafrika tuna matatizo kweli. kisha tunawalaumu wazungu kuwa wanaturudish nyuma
Hapana, mita 60 ni sheria ya nchi iliyoyungwa na haohao kina Mbowe (wabunge) kwamba isifanyike shughuli yoyote ndani ya hizo mita. Wananchi wakawaida wengi wameshaondolewa.
 
Hapana, mita 60 ni sheria ya nchi iliyoyungwa na haohao kina Mbowe (wabunge) kwamba isifanyike shughuli yoyote ndani ya hizo mita. Wananchi wakawaida wengi wameshaondolewa.
Heey pale mto kikavu ukiwa unaelekea arusha kama mnapapata vizuri ukiwa unapita ukiangalia upande wa juu kuna mwekezaji wa maua, matunda tena ama green house nyingi tuu vp yeye? Na bado kuna wakulima kila iitwapo leo wanaendelea kulima pale.
 
Heey pale mto kikavu ukiwa unaelekea arusha kama mnapapata vizuri ukiwa unapita ukiangalia upande wa juu kuna mwekezaji wa maua, matunda tena ama green house nyingi tuu vp yeye? Na bado kuna wakulima kila iitwapo leo wanaendelea kulima pale.
Sijui hilo, mi nimeonesha tu kuwa hilo ni la kisheria tu. Najua unalijua hilo pia na inawezekana kama si wewe basi ktk familia yako yuko aliyeathirika na sheria hii.
 
Sielewi mtu anawezaje kuweka green house bondeni kwenye chanzo cha mto. Bila shaka green house yenyewe iko mbali na chanzo cha mto. Na ninavyoelewa, green house inatumia kiasi kidogo sana cha maji kwa hiyo hata kama Mbowe katumia maji ya huo mto, atakuwa anatumia kiasi kidogo kama wanachotumia wananchi huko maji yanakoenda. Kwa hiyo sioni mantiki ya kumzuia Mbowe kutumia hayo maji. Matendo kama haya yanaleta picha mbaya kwenye akili za watu
 
Asilimia kubwa ya mashamba mkoani Kilimanjaro yanafika kwenye kingo za mito/ vijito.
Dhana ya uonevu au nia ovu dhidi ya mtu mmoja au kikundi fulani huonekana pale ambapo sheria hutumika dhidi yake/yao huku wengine wengi wenye kufanya vitendo kama hivyo hivyo wakifumbiwa macho.
Ingekuwa busara kama mkuu wa wilaya angetangaza kufunga mashamba yote ambayo yanatumia maji ya mito na yakiwa umbali kama wa shamba hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…