Mbowe ameishinda kauli ya kusema "vyama vya upinzani ni vyama vya msimu"

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
48,957
151,032
Tangu mfumo wa vyama vingi uanze hapa nchini,tumekuwa na vyama kadhaa ambavyo kwa nyakati tofauti vilikuwa ni vyama vikuu vya upinzani(vyama vyenye nguvu) kama vile NCCR-MAGEUZI chini ya Lyatonga Mrema na baadae CUF chini ya Prof.Lipumba.

Historia inaonyesha kuporomoka kwa vyama hivi, ni matokeo ya kazi za viongozi wakuu wa vyama hivi(Wenyeviti Taifa) kwa kushirikiana na viongozi wa chama kikongwe kuvihujumu na kuvidhoofisha kisiasa jambo ambalo limeshindikana kabisa kutokea CHADEMA chini ya Mbowe na hiki ndicho hasa kinachowaumu watu wa chama cha kijani na kupelekea mashambulizi yote haya kwa Mhe.Mbowe.

Kumbukeni hata JK aliwahi kusema vyama vya upinzani ni vyama vya msimu akiwalenga CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani ila alitoka madarakani huku CHADEMA ikiendelea kudunda(kumbukeeni hata yeye aliwanyanyasa wapinzani kwa kiasi chake).

Hivyo,japo nakiri Mbowe ana mapungufu yake kama kiongozi hasa katika kukiongoza chama kupambana na huu udikteta unaendelea leo hii,ila bado ni mtu alieweza kukioongoza chama chake na kubaki kuwa ni chama tishio kwa CCM Mpaka muda huu napoandika bandiko hili na hii ndio moja ya sifa ya kipekee alionayo Mbowe na inayostahili kuigwa na kuenziwa na yoyote yule atakaekuja kumrithi, vinginevyo chama hiki nacho kitakuja kuangukia katika lile kundi la vyama vya msimu na hii ndio agenda ya mabeberu wa chama cha kijani.

Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa nafasi ya mwenyekiti Taifa katika vyama vya upinzani, ndio hutumika kuua/kudhoofisha vyama hivi, ila kwa Mbowe inaonekana wamegonga mwamba na hivyo wakaishia kumfanyia figisufigusu wakidhani labda atasalimu amri wakaishia kupoteza muda wao na resources zao bure tu.

Msidanganyike na hizi propaganda zao.
 
Endelea kuota au unatumika ili upate mkate wako. Hebu tuamie kwa sasa Chadema kwenye serikali za mitaa imepata viti/viongozi wangapi? Ujue huko ndiyo kwenye msingi. Mwaka kesho 2020 mkipata wabunge 5 mkatambike malizieni kula ruzuku za mwisho mwisho! Kuanzia 2020 ACT ndicho kitakuwa chama kikuu cha upinzani hasa kwa kutegemea Zanzibar kama watafanya vizuri
Huoni hata aibu kuongelea huo uchaguzi fake?
 
Mimi na nani.. ili iweje?
Hamjui alikula viapo au?
Leo ndio mnaumia bado.. mliwategemea wamewatema kuwaacha mlivyo. Poleni sana.. wananchi akina mie tupo tunaangalia muvi lenu tu
Bora wameondoka wenyewe, maana wangtefukuzwa, mngesema mengi sana.
 
Hivyo,japo nakiri Mbowe ana mapungufu yake kama kiongozi hasa katika kukiongoza chama kupambana na huu udikteta unaendelea leo hii
Rafiki wewe unadhani afanye nini mbele ya bunduki, kutekwa, sandarusi za maiti baharini, vifo etc. Labda aanzishe vita ya msituni???(which is not desirable at all) unadhani afanye nini? toa suggestion please
 
sio mbaya kujifariji, ila huku mtaani siku hizi ni watu wanaona aibu kujisema ni Chadema tofauti na enzi za Dr. Slaa

tangu muungane na mafisadi mnaonekana ni wale wale tu na CCM.
 
Mbowe anawazidi watu wengi sana maarifa, Mbowe anajua siasa za field na si siasa hizi za kwenye makaratasi; Bila Mbowe siasa za upinzani Tanzania zisingekuwa zimefikia hapa zilipo; zingekiwa mochwaree.
Yaani kitendo cha CCM kuomba poo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ni ushahidi tosha.

Mbowe ni Jabari la siasa Afrika, nguli wa siasa za upinzani ..hili halina ubishi kabisa.

Mungu akulinde Mh. Mbowe, eti wanataka uachie njiani ili wapumue...
 
Back
Top Bottom