Mbowe alifanya vizuri kutosikiliza waliomuambia astaafu, akagombea, akashindwa na kuonyesha Demokrasia ipo CHADEMA

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,981
19,267
Freeman Mbowe angesikiliza watu wanaomuambia astaafu amuachie Lissu, Chadema kingekuwa ni chama ambacho kinatoa uongozi kwa kurithishana badala ya demokrasia, hii ingekifanya kuonekana bado ni mali ya Mbowe na wanaomzunguka badala ya taasisi ya wanachama wote

Sasa tunasubiri kuona kama atamuonyesha Lissu ushirikiano badala ya kumuwekea vigingi kwenye muelekeo mpya anaotaka kuipeleka CHADEMA.

Sababu bado ana nguvu sana CHADEMA licha ya kuwa ameshindwa, ana wajumbe karibia nusu wanaomuunga mkono.

Pia soma
Pre GE2025 - Freeman Mbowe akubali kushindwa, awapongeza Lissu na Heche kwa ushindi
 
Back
Top Bottom