Mbona Taifa kama halina furaha? Hofu, Chuki, mitafaruku imetamalaki

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,334
72,798
Kuna nini kimetupata? Nimejaribu kufanya utafiti wangu uchwara na kugundua Watanzania katika kipindi cha nusu nwaka huu furaha haipo kabisa, chuki kati yao iko wazi, hali ya upatikanaji wa huduma kwa wengi imekuwa ngumu, wanasiasa wamekuwa maadui tofauti na zamani wakipokuwa wanabishana kwa hoja, kwenye michezo hakuna kinachoendelea ni aibu tuu nk nk.

Ni kama tuko msibani vile, ndio maana hata sherehe za kitaifa nazo zinazuiwa. Wafanyakazi hata wale waadilifu nao ni woga tuu, huku Polisi nao wameanza kuitwa Gestapo.

Kule kwetu hali hii ya kukosa furaha na mifarakano ikitokea kwenye ukoo tunasema kuna GUNDU. Je, taifa letu nalo limepata GUNDU?
 
Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu October, zaid hasa tangu kutangazwa kwa matokeo ya urais na mwisho tangu siku ya kuapishwa rais wa sasa ambaye ukijisahau tu ukamuita majina asiyotaka kuyasikia imekula kwako, kuanzia hapo furaha ilitoweka kabisa kwa watanzania.
 
Sabotage statements.. Kauli za hivi zitakuja nyingi kwa kuwa kuna kazi inafanyika..

Tuache mzee afanye kazi, hakuna mabadiliko yasiyo na maumivu.. Tuwe wazalendo angalau kidogo. Hivi kazi kubwa anayofanya ni kwa faida ya nani?! Maana anapoteza marafiki hata kwenye chama chake lakini hajali.. Angeamua kula bata asingeshindwa!
 
Mabadiliko yoyote yenye tija huanza hivi.
 
Kweli kabisa tutakaonufaika ni sisi na vizazi vijavyo
 
Mkuu lakini kazi ya kujenga nchi sii ni ya pamoja?
Hivi unataka kuniambia familia inapojenga nyumba yao ya kuishi watu wanafarakana, kuchukiana na kukomoana kwa vile ni kipindi cha mpito cha kujenga nyumba?
 
Matunda ya kazi hua yanaonekana mda kidogo baada ya mtu kuanza kufanya kazi ila mpaka sasa amna matunda yoyote tunayoyaona na kile kidogo tunachopata nacho wanakitaka.Sijui ni kazi gani anafanya sasa.
 
Mkuu lakini kazi ya kujenga nchi sii ni ya pamoja?
Hivi unataka kuniambia familia inapojenga nyumba yao ya kuishi watu wanafarakana, kuchukiana na kukomoana kwa vile ni kipindi cha mpito cha kujenga nyumba?
Mkuu Watanzania wanapenda maisha raisi, hawataki kufanya kazi, wanapoambiwa kula kwa jasho wengi wanatahayari. Watanzania bila kujali tofauti zetu tushirikiane kujenga nchi, tuache siasa uchwala. Kuna watu walikuwa wa kwanza kuilalamikia serikali kuwa watoto wa shule wanakaa chini, leo hii kawaulize wamesaidiaje upatikanaji wa madawati? hamna kitu kabisa.
 
Reactions: Ame
Siyo kila mabadiliko yawe na maumivu, au labda maumivu unayoyazumngumzia ni kuwafungulia wanasiasa mashtaka na kuwapeleka korokoroni? kuzuia mikutano ya wanasiasa wa upinzani? kuzuia hata mahafali ya ndani? kutoa kauli tata na chonganishi kwa raia?, ... nadhani hayo ndio maumivu unayoyasema.

Nadhani kazi kubwa anayofanya ni kukandamiza demokrasia ya nchi HURU , na anafanya kwa faida ya chama chake cha kijani kama kinavyotaka bila kusahau fikra zake zinavyomtuma.
 
Kwani we hupendi maisha rahisi,?
unakamuliwa kodi yako mpaka unashindwa kupumua usitake maisha rahisi.?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…