Reginald Mengi ni mfanyabiashara mkubwa sana hapa nchini. ndiye mwenyekiti mtendaji na mmiliki wa makampuni ya IPP yanayomiliki ITV, RADIO ONE, GAZETI LA NIPASHE na mambo mengi hapa nchini. alishawahi kulalamikia watawala wakuu wa nchi kama ifuatavyo?
1. Enzi za MKAPA: alilalamikia sana kukosa hoteli ya KILIMANJARO ambayo alipewa mfanyabiashara kutoka Uarabuni. Mengi alidai kuna rushwa ktk utawala wa enzi hizo na ndiyo maana aliikosa hiyo fursa.
2. Enzi za KIKWETE: alilalamikia kuwa fursa za kibiashara wanapewa wachache wanaojua kutoa rushwa. akawataja akina Manji na wengine kuwa ni MAFISADI PAPA. aliilaumu serikali ya Kikwete kwa kulea rushwa na upendeleo.
Sasa yuko JPM, sijaona maoni ya mzee Mengi. hii inashiria nini? hamkubali JPM pengine anamwona mbabaishaji AU yeye Mengi ndo msanii AU anampa muda ndo atoe yake ya moyoni?