Mbona bei za vyakula karibu vyote zimepanda ghafla?

bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,015
4,982
Habari wana JF,

Jana nimeenda dukani kununua bidhaa mbali mali za nyumbani, sasa basi nilichokutana nacho ni kuwa bidha karibu zote zimepanda bei kama ifiatavyo;

Sukari kilo kutoka 2400 hadi 2600 sehemu nyingine 2800.
Mchele kilo kutoka 2400 hadi 2800 na kuendelea.
Sabuni ya jamaa mche kutoka 2500 hadi 3000.
Mafuta ya kupikia nayo yamepanda bei.
Hata kahawa ambayo nayo hupenda kunywa mara nyingi nayo imepanda bei.


kuna baadhi ya nchi bidhaa hazipandi bei kiholela lela hata mkate tu ukipanda wanannchi wanaandamana kupinga ongezeko hilo na serikali yao huwasikiliza mara moja lakini hapa kwetu kazi ya serikali ni kupiga marufuku tu lakini sio kumsaidia mwananchi

Wakuu hivo ndivo vitu nilivonunua jana nikakuta vyote vimepanda bei sasa sijajua kwa upande wa vitu vingine pamoja muelekeo wa maisha yetu watanzania tunaelekea wapi.

Naona hata serikali nayo imeshindwa kupunguza kodi ili bidhaa nazo ziweze kushuka, wananchi wa kawaida ndo wanaoumia.
 
Porojo tu hizi. Jana nimenunua...
Sukari kilo 2500
Mchele Kilo 2000
Sabuni jamaa mche 2000
Mafuta Sunbelt 5lts 24,000

Punguza uongo mkuu.
sina sababu ya kusema uongo hapa silipwi na yoyote,
kwa mujibu wa mwenye duka mzigo umepanda bei toka jana maana ndo alifuata mzigo na kuja nao
 
sina sababu ya kusema uongo hapa silipwi na yoyote,
kwa mujibu wa mwenye duka mzigo umepanda bei toka jana maana ndo alifuata mzigo na kuja nao
upo mkoa gani na mtaa gani? anzia hapo ili tuende sawa, kwa maana bei ya mchele kule rujewa ni tofauti na bei ya kimara
 
Kweli kuna baadhi ya vitu bei imepanda na sababu kubwa, ni kupanda kwa bei ya petrol. Lakini sababu nyingine ni kwamba, mvua zinzoendelea kunyesha zimeharibu miundombinu katika barabara nyingi, hii pia imechangia maana ni magari machache yanayoweza kusafirisha mazao hadi kufikisha maeneo ya mjini
 
Bidhaa iliyotangazwa kupanda ni nyanya hata Mimi nilishtuka juzi naenda sokoni nakuta vinyanya vitatu vidogo vinauzwa jero
 
hapo utapishana na wachangiaji sababu hujaweka location yako na wachangiaji wanachangia kutokana na location yako wengine wako kishisha wenye mafuta huko wana stock za mwezi wa kwanza
Swali hili kaliona muanzisha mada au anajibu Kwanza ya kuchagua yenye alama chache? Naona analalamika akiitaja taja serikali anahitaji siasa hapa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom