kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,318
- 4,101
Kwa takribani zaid ya miaka saba sasa jina la Nguli wa uneni na ulumbi wa kiswahili fasaha kupitia maghani yake yanayojazwa na viitikio vya bongo fleva limekua miongoni mwa wasanii wenye mashabiki na wanaopata deals mbalimbali za ubalozi na maonyesho. Pamoja na kughani kwa ufasaha pia amekuwa mwafrika kwa maana ya kujaribu kufanana na mwafrika halisi aliyeishi tangu enzi zile.
Licha ya kuwa msanii mwny uwezo mkubwa katika sanaa ya kughani, msanii huyu ni MNAFIKI,MCHUMIA TUMBO na MUOGA yawezekana kuliko msanii yeyote kwa wasanii wote wa nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara.
Amekuwa akijitahidi kuimba nyimbo za kukosoa serikali lakini ukitazama kwa umakini mitazamo yake katika kuzungumzia masuala mbalimbali ya utendaji wa serikali amekuwa akiipigia upatu serikali ila katika wimbo wake wa sizonje anaonyesha kumuonya sizonje juu ya dosari zilizopo katika serikali.
Sasa Mrisho mpoto mfumo unaoukosoa dosari zipo kwny serikali au kwa wananchi?? Umekuwa mbayuwayu huelewek ni mashariki au magharibi wataka kuelekea,maisha yako ktk sanaa na ushabiki wako pasi na kuacha ukosoaji ktk nyimbo zako kwa pamoja nimegundua umejawa na UNAFIKI.
Juzi ulimkingia kifua Makonda hukusema kwa sauti juu ya uvamizi wa clouds na dosari za swahiba wako aliyeghushi vyeti ila kwa unafki uliokujaa pale juzi ukawahadaa watu eti una taharuki baada ya kukamatwa kwa Roma??....
Unanunulika kwa urahisi sana na nimegundua wewe ni msanii muoga sana pia unapenda sana kujipendekeza kwa watawala ila nikupe tu angalizo, kama Nape ameyeyushwa kirahisi utakuwa ww?? Kwa unafiki uliojaa eti unatembea peku wakati upo mlimani city,kwenye gari na airport tu wakati huko kuna tiles,kama ww kwel unataka madini asilia ya udongo na unaamini utayapata kwa kutembea peku katembee peku pale buguruni sokoni,tandale,kigogo na uwanja wa fisi.mbona juzi pale central kwny ishu ya Roma ulivaa viatu??.huko unapotembea peku hakuna udongo kuna tiles.
Nilitarajia ww utakuwa ni sauti ya wasanii utakayesema nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe pasipo hofu yoyote kwani ukiachilia mbali ujuvi wako wa lugha,Wewe ni msanii mwenye umri mkubwa kwa sasa kuliko wenzako wote. Una tabia za uswahiliswahili wa kutukuza watawala na kujikomba kwao huku ukiwakingia kifua kwa maovu yao.
Anguko lako la kisanaa linakuja usipojiangalia kwani mashabiki zako wanapungua kila uchao.