Kuelekea 2025 Mbinu za wizi wa kura zinazotumiwa na CCM zabainika; ni hizi hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
23,518
21,544
Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya uandikishaji wa watu watakoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, CHADEMA wanahamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha lakini CCM wanaendelea kuimarisha mbinu zao za wizi wa uchaguzi. Kama ulikuwa huju mbinu za wizi wa uchaguzi zinazotumiwa na CCM, hasa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na hatimaye uchaguzi mkuu mwaka 2020, basi mbinu hizo ni kama ifuatavyo:

1. Ulegezaji wa masharti ya kujiandikisha
Ulegezaji wa masharti ya kujiandikisha uliobuniwa na CCM kwenye uchaguzi wa mwaka huu, haujawahi kutokea. Wameweka mfumo huu ili wawatumie wafuasi na makada wao kujiandikisha mara nyingi kadri iwezekanavyo ili kuongeza idadi ya kura zao na kujishindia uchaguzi kiulani. Kwa mfumo huu, ambao mtu anatakiwa kutaja tu umri na kutia saini kwenye daftari la uandikishaji bila kuhitajika kwanza kutambuliwa na uongozi wa mtaa/eneo husika, CCM wamepiga hatua kubwa sana katika wizi wa uchaguzi wa mwaka huu.

Mtu mmoja anaweza kujiandikisha hata mara 1000 kwenye vituo tofauti. Kwa mwanya huu, makada wa CCM makumi kwa maelfu wanazunguka kila kituo kujiandikisha bila wasiwasi wowote. Kwa mfano makada 700 wa CCM wakijiandikisha kwenye vituo 1000 watakuwa wameongeza idadi ya kura hewa 700,000. Fikiria mgombea wa CCM anakuwa na akiba ya kura hewa 700,000 mgombea wa CHADEMA au wa chama kingine cha upinzani anashindaje kwa mfano?

2. Kuteua makada wa CCM kusimamia uchaguzi
Tume ya uchaguzi huwatumia wakurugenzi wa halmashauri, ambao ni makada maarufu wa CCM kusimamaia uchaguzi. Aidha, wakurugenzi hawa huhusika moja kwa moja kuwateua wasimamizi wa vituo vya kupigia kura. Tukumbuke uchaguzi unapoitishwa, wakurugenzi, huwaalika “wananchi” kutuma maombi ya kusimamia uchguzi. Hapa sasa ndio patamu!

Kinachofanyika katika zoezi hili la uteuzi ni kiinimacho tu. Kabla ya hao wanaoitwa wananchi kuandika barua za kuomba kazi ya muda ya kusimamia uchaguzi, makada wa CCM tayari wanakuwa wameishaelekezwa kuandika baraua kwa wingi sana na kwa kuwa wanafahamika, wakati wa uchambuzi wa majina ya watakaosimamia uchaguzi, 99.99% ya “wananchi” wanaoteuliwa, ni makada wa CCM. 0.01% inayobaki kukamilisha 100% ya wasimamimizi, huwaendea walimu, tena wale ambao ni makada wa CCM. Kwa hiyo, utaona kwamba vituo vya kupigia kura vinakuwa vimesheni makada wa CCM tupu. Hapo sasa nieleze nini zaidi? Si tayari CCM wamejihakikishia ushindi?

3. Kupiga kura baada ya kura
Mwaka 2020, wasimamizi wa vituo vya kupigia kura, wengi wao wakiwa walimu na makada wa CCM, walishurutishwa na wakurgenzi wa halmashauri kuwapigia kura wagombea wa CCM baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika na vituo kufungwa. Katika halmashauri moja nilishuhudia wasimamizi wa vituo wakifungiwa kwenye chumba maalumu ambapo kila mmoja alielekezwa kuwapigia kura wagombea wa CCM kwa idadi iliyoelekezwa na mkurugenzi wa halmashauri ili kuongeza idadi ya kura.

Timu ya ushindi iliyoteuliwa na mkurugenzi ilikuwa akiwasiliana na wasimamizi wa vituo na kuwauliza kama wagombea wa CCM wameshindwa au kushinda kwa asilimia ngapi. Katika kituo kimoja, mgombea wa CCM alipata 51% ya kura zilizopigwa. Mkurugenzi alikasirika sana akamuagiza msimamizi kuboost hizo kura hadi 99% kwa kuongeza idadi ya kura za mgombea wa CCM bila kupunguza zile za wagombea wa upinzani.

Mbinu hii hutumika pale kunapokuwa na idadi ndogo ya watu waliojiandikisha na idadi ndogo zaidi ikajitokeza siku ya kupiga kura. Hata ikiwa idadi ya “waliopiga kura” itatofautiana na idadi ya waliojiandikisha, potelea mbali (Nape, 2024). Hii mbinu ilitumika zaidi mwaka 2019 baada ya wagombea wote wa CHADEMA kujitoa na kubakiwa wagombea wa CCM na vyama vingine ambavyo ni matawi ya CCM, hivyo kupelekea hata wapiga kura wa CCM kutojitokeza kupiga kura, baada ya wagombea wa chama chao kuwa na uhakika wa ushindi.

1729420280636.png
Wananchi wakipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura (Chanzo: Mtandao)

4. Kuandika idadi bandia ya kura zilizopigwa
Hii ndio ile mbinu aliyoisema Nape Nnauye na ndiyo iliyotumika kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020. Katika mbinu hii, kura zinazopigwa ndani ya vyumba vya kupigia kura hazihesabiwi. Kinachotokea ni kwamba mkurugenzi wa halmashauri, ambaye ni returning officer (RO) hujifungia kwenye chumba na timu yake ya ushindi na kutengeneza kura bandia kwa kila kituo cha kupigia kura (kulingna na idadi ya wapiga kura) akimchuanisha kwa mbali mgombea wa CCM na wagombea wa vyama upinzani.

Kwa mfano, ikiwa kituo A cha kupigia kura kina jumla ya wapigakura 300 na wagombea wa vyama vya CHADEMA, CCM, ACT, CUF na CHAUMA, kura za bandia kwa wagombea zinaweza zikatungwa kama ifuatavyo:

CCM =290
CHADEMA =7
ACT =2
CUF =1
CHAUMA = 0

Mfumo huu wa wizi hutumiwa kwenye kila kituo cha kupigia kura kwa kumpaisha mgombea wa CCM mbali kabisa na wagombea wa vyama vingine. Kwa mfano wa hapo juu, mgombea wa CCM anakuwa ameshinda kwa 96.7%.

Wizi huu hufanikishwa na mtendaji wa kata, ambaye kwa nafasi yake hupewa cheo cha Asisitant Returning Officer (ARO). Watendaji hawa hupita kila kituo na kukabidhi matokeo bandia kwa msimamizi wa kituo kwa kutumia mbinu ya kujificha mahali na kumuita msimamizi aje kuchukua matokeo. Polisi pia hutumiwa kupeleka matokeo kwa wasimamizi.

5. Matumizi ya polisi wanaolinda vituo vya kupigia kura
Aghalabu polisi hutumiwa kuwatoa nje wagombea wa upinzani ili CCM wapate kuingiza kura bandia kwenye masanduku ya kura. Kinachotokea ni kwamba msimamizi wa kituo cha uchaguzi (ambaye ni kada wa CCM) huanzisha ugomvi wa lazima dhidi ya mawakala wa vyama vya upinzani na kisha kuwaita polisi kuja kutuliza ghasia. Polisi wanapokuja huwachota mawakala wa upinzani na kuwapakia kwenye gari, hivyo kumuachia mwanya msimamizi wa kituo kuingiza kura bandia kwenye masanduku.

Baadaye polisi huwaachia huru wale mawakala kurudi ndani ya vyumba vya kupigia kura. Kufuatia, kadhia hii, mawakala wa vyama vya upinzani hugoma kusaini hati za uchaguzi wakati wa kufunga vituo lakini kugoma kwao hakusaidii chochote kwani tayari uchaguzi unakuwa umeibiwa na CCM.

6. Kuwazubaisha mawakala
Wengi wa mawakala wanaosimamia kura za wagombea wa upinzani, huletewa chakula na mgombea husika. Ikiwa mgombea atachelewa kuleta chakula, fedha zilizotolewa na mkurugenzi hutumika kuwanunulia chakula mawakala wote bila kuwabagua kivyama. Wakati mawakala wote wameenda kula, msimamizi wa kituo cha kupigia kura hutumia mwanya huu kuingiza kura bandia kwenye masanduku ya kura. Ikifika muda huu wa kula, wakala wa CCM naye huzuga kuambatana na mawakala wa upinzani kwenda kwenye chakula huku akiwa anafahamu fika mchezo utakaoendelea nyuama ya pazia.

7. Kuwanunua au kuwateka wagombea wa upinzani
Mtindo wa ununuzi wa wagombea wa upinzani hauna haja ya kuueleza hapa kwani kila mtu anafahamu jinsi wagombea wa upinzani wanavyonunuliwa kujitoa kwenye uchaguzi au kupotea siku ya kurudisha fomu.

8. Ulaghai na kuficha taarifa za uchaguzi au taarifa binafsi za wagombea
Aghalabu CCM hutumia mbinu ya kuficha taarifa za uchaguzi kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi ambayo huteuliwa na Rais, ambaye naye huwa ni miongoni mwa wagombea. Hii ni sheria ya ajabu kabisa katika nchi hii ya kusadikika.

Katika ngazi ya kata, watendaji wa kata hutumika kuficha fomu za wagombea wa upinzani kwa makusudi au kujificha siku wagombea wa upinzani wanaporejesha fomu. Tukumbuke kuwa watendaji wa kata kwa sasa hivi huajiriwa kwa misingi ya kiitikadi. Watendaji wanaoajiriwa kwenye kata sasa hivi hupangiwa vituo moja kwa moja kutoka makao makuu ya CCM, Dodoma. Kwa hivyo, hawawezi kwenda kinyume na maagizo au maelekezo ya CCM hata siku moja.

N.B: Ikumbukwe kwamba siku chache kabla ya tarehe ya uchaguzi wasimamizi wa vituo vya uchaguzi kwenye kila kata huitwa kupewa semina ya wizi na kiongozi wa ushindi aliyeteuliwa na mkurugenzi wa halmashauri.

Nawasilisha
 
View attachment 3130687

Katiba mpya, katiba mpya,tutaburuzwa kama maksai!
 
Back
Top Bottom