Muaza saadala
New Member
- Aug 28, 2022
- 2
- 0
MBINGU KUMI NA NNE
Tanzania ni binti mrembo wa Kiafrika ambaye kwa bahati mbaya alifiwa na wazazi wake pamoja na mdogo wake wa kiume akiwa na umri wa miaka kumi na mitano tu.Ilichukua masaa kadhaa tu kumfanya binti huyu mrembo kuuitikia upweke uliobisha hodi ndani ya nafsi yake na kumfanya asiione tena thamani ya kuishi katika dunia hii yenye sura ya ajabu.
Liishalo ni dogo kuliko linalokuja,ndivyo ilivyokuwa kwake baada ya mawazo haya mabaya kumuathiri kisaikolojia na kupelekea kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya akiwa na umri wa miaka kumi na Saba pekee. Miezi kadhaa mbele, mambo yakawa mabaya zaidi pale binti huyu ambaye kwa wakati huu mwili wake ulinyong'onyea mithili ya ng'ombe wa kiangazi, alipojikuta akiwa na ujauzito ambao hakuutarajia kabisa kutokana na mlolongo wa matatizo yaliyokuwa yakimkabili. Hili likawa funzo kubwa kwa binti huyu huku nafsi yake ikimsihi asimame na kupambana kwani asipofanya hivo hakuna atakaye kuja kusimama kwaajili yake kwa wakati huu Tanzania hakuwa hata na nguzo ya kuegama Wala mahala pa kusimama baada ya baba yake mdogo kumdhulumu Mali zote zilizoachwa na wazazi wake.
Ilikuwa tarehe 21 mwezi wa Tisa mwaka 2021 majira ya saa kumi na mbili jioni huku kiza taratiibu kikianza kuita,upepo ukilibembeleza anga ambalo sasa lilikuwa likiagana na jua,ndipo sauti nyembamba ya mtoto mchanga iliskika. Ndio! Tanzania alijifungua salama mtoto wa kiume na kuamua kumpa jina zuuri "Africa",jina ambalo ndilo likikuwa jina la baba yake mzazi kwa wakati wote huu alikuwa akipingana na Ibilisi ambaye alimwambia kwa sauti ya kumtoa nyoka pangoni "mtupe huyo mtotoo!" Lakini akawa jasiri na kuishinda nafsi hii.
Ulipofika mwaka 2022, aliskia taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa serikali imeamua kuanzisha utaratibu maalumu kwa mabinti walioachishwa shule kutokana na mimba za utotoni kwa kuwapa fursa za kujiendeleza kielimu.Hii haikuwa fursa ya kuacha kwa Tanzania japo alikuwa na changamoto nyingi lakini hazikumzuia yeye kujiandikisha katika shule ya sekondari Mama Samia.
Akiwa hapo alibahatika kupatiwa msaada wa kifedha kwa ajili ya kujikimu na matumizi ya mtoto pia.Sasa Tanzania yupo kidato Cha pili na mwakani anatarajia kuhitimu kidato Cha nne huku akiwa tayari kutimiza ndoto zake za kuwa mwandishi wa habari.
"KAMA TUNAHITAJI MABADILIKO HATUNA WA KUMTUPIA LAWAMA BALI NI LAZIMA TUKUBALI KUBADILIKA KWANZA SISI WENYEWE."