Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,645
Juzi tarehe 2/2/2023 Mjumbe wa Shina namba 9 Mbezi Beach B Bw. Daudi anasema alipigiwa simu akiambiwa kuna mtu ambaye amefia kokoni, ambapo alipofika eneo la tukio akakuta kichwa cha mwanaume huyo kimetenganishwa na kiwiliwili.
Tukio hilo linaonekana kufanywa siku mbili au tatu kabla kutokana na mwili kutoa harufu ambapo Bw. Daudi aliwapigia simu polisi na serikali za mitaa Mbezi A (tukio limetokea katikati ya Mbezi Beach A na B) na kusimamia mwili huo mpaka polisi walipofika.
Bwana Daudi aendelea kueleza tukio hilo siyo la kwanza, kulishatokea tukio jingine maeneo ya kwa Rwakatare, lakini pia hapo ulipokutwa mwili wa mwanaume walishawahi kukuta mwili mwingine wa mwanamke ambaye mwili wake naye ulikutwa umeshaharibika sana ambapo ilibidi wamzike hapo hapo, na kusema kuwa eneo hilo ni hatarishi hasa wakati wa usiku, na wezi wa nyaya za TTCL wamewahi kutumia eneo hilo kama kichaka chao.
Bw. Daudi na mashuhuda wengine wameiomba serikali kukata miti eneo hilo, msitu ufyekwe ili kuwa salama kwa wakazi hao kutokana na matukio hayo ya kikatili pamoja na mto kusafishwa ili maji yaweze kupita vizuri yasiharibu makazi ya watu pindi mvua zinaponyesha.
Wasafi Media