Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 541
- 532
Ni kwamba Novemba 25, 2024 Saa 2:00 Usiku huko Mtaa wa TEKU viwandani Jijini Mbeya, mtoto Chloy Ramadhan [04] alifariki dunia baada ya kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake mzazi aitwaye Ramadhan Tembo Mwakilasa [28] akishirikiana na mama yake wa kambo aitwaye Mariamu Charles Mwashambwa [28] wote wakazi wa TEKU viwandani.
Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ukatili na unyanyasaji kwa kumuadhibu mtoto baada ya kujisaidia kwenye nguo alizokuwa amezivaa.
Jeshi la Polisi linawataka wazazi/walezi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi dhidi ya watoto pindi wanapokosea na badala yake watumie njia sahihi na salama kuwafundisha au kuwaelekeza bila kusababisha madhara.
==============
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Ramadhan Tembo Mwakilasa [28] na Mariamu Charles Mwashambwa [28] wote wakazi wa TEKU viwandani Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Chloy Ramadhan [04] kwa kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili.
Ni kwamba Novemba 25, 2024 saa 2:00 usiku huko Mtaa wa TEKU viwandani Jijini Mbeya, mtoto Chloy Ramadhan [04] alifariki dunia baada ya kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake mzazi aitwaye Ramadhan Tembo Mwakilasa [28] akishirikiana na mama yake wa kambo aitwaye Mariamu Charles Mwashambwa [28] wote wakazi wa TEKU viwandani.
Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ukatili na unyanyasaji kwa kumuadhibu mtoto baada ya kujisaidia kwenye nguo alizokuwa amezivaa.
Jeshi la Polisi linawataka wazazi/walezi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi dhidi ya watoto pindi wanapokosea na badala yake watumie njia sahihi na salama kuwafundisha au kuwaelekeza bila kusababisha madhara.
Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya