Mbeya ni namba 3 kuchangia Pato la Taifa ila haipo kwenye 10 bora mapato ya TRA. Hii kiuchumi imekaaje?

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,582
14,167
Habari ndugu wadau.

Kuna jambo la kuelimishana hapa kwa wabobezi wa Masuala ya Uchumi.

Inakuaje Mkoa wa Mbeya ambao uko namba 3 Kuchangia Pato la Taifa yaani GDP na pia iko namba 4 Kwa kuwa na watu wenye kipato cha juu yaani Per Capita Income yet makusanyo yake ya TRA ni only Bil.69 kwa Mwaka huku ikizidiwa na Kagera ambayo ni Kati ya Mikoa inayotajwa kuwa ni Maskini?

Kiuchumi hii inakuaje ndugu wabobezi. Nauliza hivi kwa sababu Mikoa Mingine Inayochangia GDP kubwa pia inachangua Mapato mengi kuko TRA.

Scenario hii ya Mbeya iko pia Mkoa wa Ruvuma. Nahisi TRA hawakusanyi mapato ya Kutosha 👇

20221025_114623.jpg
Screenshot_20221025-203055.png
 
Hizo figure sijui wanazitoa wapi! Ukienda Mbeya mjini kwa mfano, nyumba ni zile zile za udongo na zimekuwapo miaka 30 iliyopita. Watu hawajengi. Wanaishi kwenye nyumba za urithi. Wanapata ela ya kula tu na ya kupanda Bajaji.

Uchumi wa Mbeya hasa manispaa bado sana

Kuna bidhaa fulani tulikuwa tunauza, you cant imagine, ile bidhaa ilikuwa na soko kubwa kwa mkoa wa singida kuliko mkoa wa Mbeya!
 
Maana yake mzunguko wa hela ni mdogo. Uchumi wa mkoa huo ni agrarian, siyo as indusrious.
Industrialized ni Dar na Arusha.
Mingine ni agrarian.
Kagera kuna Viwanda gani vya kuzidi Mbeya?

Mzunguko wa Hela ni mdogo wakati Mkoa uko namba 3 kwenye GDP?

Pia Mbeya iko top 5 kwenye Mikoa yenye mapato makubwa ya Halmashauri zake?

Why TRA revenues hazi reflect uhalisia?
 
Hizo figure sijui wanazitoa wapi! Ukienda Mbeya mjini kwa mfano, nyumba ni zile zile za udongo na zimekuwapo miaka 30 iliyopita. Watu hawajengi. Wanaishi kwenye nyumba za urithi. Wanapata ela ya kula tu na ya kupanda Bajaji.
Uchumi wa Mbeya hasa manispaa bado sana...
Mbeya Mjini wapi ambako nyumba ni zile zile?
 
Kagera kuna Viwanda gani vya kuzidi Mbeya?

Mzunguko wa Hela ni mdogo wakati Mkoa uko namba 3 kwenye GDP?

Pia Mbeya iko top 5 kwenye Mikoa yenye mapato makubwa ya Halmashauri zake?

Why TRA revenues hazi reflect uhalisia?
Wew kagera ushawahi kufika kwanza
Kagera kuna viwanda vikubwa sana zaidi ya 10...kimoja wapo ni kagera sugar chenye irrigation scheme kuliko vyote Africa...

Hebu soma hapa...

Ninachofahamu, kuna tofauti kati ya GDP, kipato, na mapato.

Kuna utajiri wa eneo husika, utajiri wa watu na mapato ya eneo husika.

Watu wanaweza wakawa na kipato kikubwa ila makusanyo ya kodi yakawa hafifu.

Pia eneo husika linaweza likawa na utajiri mkubwa ila ukawa unamilikiwa na wachache, na hivyo pakawa na umaskini mkubwa na mapato kidogo
 
Kagera kuna Viwanda gani vya kuzidi Mbeya?

Mzunguko wa Hela ni mdogo wakati Mkoa uko namba 3 kwenye GDP?

Pia Mbeya iko top 5 kwenye Mikoa yenye mapato makubwa ya Halmashauri zake?

Why TRA revenues hazi reflect uhalisia?
Industrious haimaanishi viwanda.

Inamaanisha uchumi ambao fedha inatumika kupata maisha.

Kwa mfano, kijiji kikiwa na mashamba ya mahindi na kijiji kikiwa na hoteli za kitalii, kijiji chenye hoteli kipo more industrious.

Wafanyakazi watakatwa income tax, hoteli itakatwa corporate tax, watalii/wageni watanunua huduma za usafiri etc.

Kijiji chenye mashamba ya mahindi itauza baadhi ya mahindi na kula baadhi, ingawa thamani ya jumla ya mahindi inaeza kuwa sawa na thamani/pato la hoteli. Ila kodi zitatofautiana.
 
Kama hiyo ndio hoja yako how comes Mbeya ni namba 3 Kwa watu wake kuwa na higher income yaani per Capita income?
 
Ninachofahamu, kuna tofauti kati ya GDP, kipato, na mapato.

Kuna utajiri wa eneo husika, utajiri wa watu na mapato ya eneo husika.

Watu wanaweza wakawa na kipato kikubwa ila makusanyo ya kodi yakawa hafifu.

Pia eneo husika linaweza likawa na utajiri mkubwa ila ukawa unamilikiwa na wachache, na hivyo pakawa na umaskini mkubwa na mapato kidogo
Kwa nini? Labda nature ya activity husika zinakuwa ngumu kukusanya mapato tofauti na baadhi ya activity kama migodi.
 
Back
Top Bottom