Mbeya: natafuta vifaranga wa samaki na watotoleshaji wa vifaranga wa kuku!.

Kajole

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,668
1,644
Rejea post yangu hii Kati ya Songea na Singida ni mkoa upi mzuri kwa mtu anaetaka kuishi na kujishuhurisha na ufugaji na kilimo?.

Nilibahatika kuzunguka msimu wa pasaka ili kujifunza na kuangalia fursa zilizopo ktk sekta hii!. Ukweli nmejifunza mambo mengi sana na lazima niyaweke ktk utekelezaji.
Safar yangu nlianzia Mbeya(ndiko niliko) nkapita makambako,njombe,songea,Lindi,mtwara,dar,morogoro na iringa then nkafika kwetu Mbeya!. Katika safar yangu hii nilipitia vijiji mbalimbali AMBAVYO WADAU humu JF walishauri either kwenye hiyo post or through PM hivyo NAWASHUKURU sana wadau maana nimegundua humu ndani kuna watu wa aina tofauti tofauti wanaojua mambo mengi mazuri maana maeneo yoooote niliyoelekezwa ni mazuri na yana fursa za kukutoa kimaisha.
OK nisizungumze sana hoja yangu ni kuwa: nimebahatika kupata eneo la ekari 3
(210 squàre metres) lipo Mbeya eneo linaitwa Inyala,kwanini Inyala?
1. Bei nzur sana kwa ekari 150000 mpaka 250000
2. Ni 3km kutoka barabara kuu ya Dar - Zambia na 20 km kutoka mbeya mjini
3. Access ya usafiri ni kubwa yaan kifupi ni 24 hrs kwenda Dar au Mbeya
4. Umeme,maji na networks(mitandao yote H+)
5. Hali ya hewa si joto wala si baridi sana moderate hii inapelekea mazao mengi kukubali pia wanalima mwaka mzima maana wana mifereji ya maji inayopita mashambani walioutoa kwenye MTO mkuu unaopita pembezoni mwa kijiji
Na mengine mengi.

Sasa basi mi nmeanza utekelezaji kwa kuzungusha fensi shamba lote(fensi ya waya wa senyenge-sijui ndo inavyoitwa) pia tumejenga banda la mabanzi tunalala humu navyojiandaa kujenga nyumba ya kudumu. Pamoja na yote hayo pumzi ya kifedha imekata kama ujuavyo mitaji tunaunga unga tu sasa basi nmeamua:
a. Kuku wa kuanzia ninunue mayai na nitotoleshe hata vifaranga 100 wakuanzia ili kupunguza gharama
b. Nifuge na samaki wachache kama 1000 hivi
c. Nilime na zao la muda mfupi ambalo si sumbufu ktk kulihudumia.

MSAADA WENU:
1. Nani alie mbeya anaetotolesha vifaranga?
-bei gani anafanya kwa kifaranga?. Mayai ni yangu yeye ananichaji mashine na umeme tu.
2. Muuzaji wa mbegu za samaki hapa mbeya. Anauzaje? Pia huyu napenda awe mshauri pia ktk mradi huu
3. Zao gani ni zuri kulilima kibiashara ukizingatia maelezo hapo juu yaani:
i. Liwe la muda mfupi ili nilitumie kupata kipato cha kuendesha maisha navyosubir maini project iwe matured
ii. Lisiwe zao sumbufu yaan sio lile ambalo linahitaji uangalizi kama mgonjwa wa ICU
iii. Liwe na soko angalau

Asanteni sana
 
Habari Mkuu,hongera sana.Kama upo Inyala kuna mtu anatotolesha vifaranga kwa bei nafuu sana.Npm nikuelekeze.Pia kuhusu samaki nipm pia nikuelekeze sehemu ya kupata kama umeshaandaa bwawa la kufugia itakuwa nzuri zaidi ila ni samaki jamii ya Sato na Sangara.
 
Habari Mkuu,hongera sana.Kama upo Inyala kuna mtu anatotolesha vifaranga kwa bei nafuu sana.Npm nikuelekeze.Pia kuhusu samaki nipm pia nikuelekeze sehemu ya kupata kama umeshaandaa bwawa la kufugia itakuwa nzuri zaidi ila ni samaki jamii ya Sato na Sangara.
Asante mku,nmeshakuPM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom