Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

game over

JF-Expert Member
Jan 1, 2016
10,656
24,543
Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city, hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla ni typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.

IMG_5686.jpg

Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)

IMG_5671.jpg

Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

IMG_5683.jpg
Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

IMG_5688.jpg
Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako . Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

IMG_5688.jpg

IMG_5670.jpg

IMG_5667.jpg

IMG_5669.jpg

IMG_5678.jpg
 
Attachments

  • IMG_5687.jpg
    IMG_5687.jpg
    146.2 KB · Views: 47
  • IMG_5683.jpg
    IMG_5683.jpg
    296.3 KB · Views: 56
  • IMG_5682.jpg
    IMG_5682.jpg
    310.9 KB · Views: 56
Usipangie watu Maisha,wewe ongea unayotamani yawe vinginevyo pita kushoto..

Mbeya ya Leo is way better than it used to be in 2010 wakati ikitangazwa kuwa Jiji..

Njoo 2025 pia kuandika utopolo wako maana by that time Barabara Kuu njia 4 itakuwa imeisha,Barabara za mitaa km 27 zitakuwa zimeisha na ujenzi wa Stand kubwa za Kisasa utakuwa unaendelea..
FB_IMG_16860630937007527.jpg

Njia 6 Kwa Sasa haipo sana sana Kuna mradi wa BRT mbeleni na njia ya Sasa ndio itakuwa reserved Kwa Ajili ya BRT..

Mbeya ipi ambayo watu hawajengi Makazi ya Kisasa? Wewe sema Serikali iongeze Kasi ya kupima Mji..

Kitu pekee nachokuunga mguu ni Chuo Cha Kilimo na JKT hapa Uyole wapishe waende Wilayani hayo maeneo yapimwe na yagawiwe viwanja kama ilivyo Kwa Forest au Iwambi Mpya,hakuna Cha NHC,hao NHC wakajenge Dodoma huko.
20230615_130920.jpg
 
Usipangie watu Maisha,wewe ongea unayotamani yawe vinginevyo pita kushoto..

Mbeya ya Leo is way better than it used to be in 2010 wakati ikitangazwa kuwa Jiji..

Njoo 2025 pia kuandika upuuzi wako maana by that time Barabara Kuu njia 4 itakuwa imeisha,Barabara za mitaa km 27 zitakuwa zimeisha na ujenzi wa Stand kubwa za Kisasa utakuwa unaendelea..View attachment 2656232

Kati ya haya niliyoyaandika kuna hata moja lisilo la kweli?
Nimekuwa mbeya for years mzee tangu nipo sekondari. Kama hakutakuwa na namna tofauti ya kufikiria na kufanya mambo basi hakuna cha 2025 wala 2050 mzee.
Mji wa mbeya ni mji wa hovyo sana, mno.
 
Hapo hakuna jipya uliloandika sana sana uko uninformed ,Mbeya Ina Master Plan yake ambayo ilizinduliwa na Waziri na pia Kuna kujenga upya maeneo ambayo halijengwa kama Slums and so any new developments inafanywa Kupitia hiyo..

Mojawapo ya uongo ni kusema eti Mbeya hakujengwi Nyumba za Kisasa 😁😁
 
Hapo hakuna jipya uliloandika sana sana uko uninformed ,Mbeya Ina Master Plan yake ambayo ilizinduliwa na Waziri na pia Kuna kujenga upya maeneo ambayo halijengwa kama Slums and so any new developments inafanywa Kupitia hiyo..

Mojawapo ya uongo ni kusema eti Mbeya hakujengwi Nyumba za Kisasa

Master plan ?, eti umesema master Plan ?
Hebu niambie Masterplan itafanya nini na Mbalizi? What will masterplan do with Iwambi na makunguru na Airport ? Uyole? Ilemi?
Ule mji ushakosewa. Hakuna kitu kitafanyika.
Nyumba za kisasa zinajengwa wapi ? Forest mpya na Iwambi?
Elewa , naijua mbeya nje ndani.
 
Kwamba hiyo masterplan inahusisha ujenzi wa fremu za kupangisha CBD?
Kwanini halmashauri ya mji wa mbeya inapenda sana Fremu ?
IMG_4462.jpg
 
Master plan itazipanga upya hizo slums Ili kwanza ziwe accessible na Huduma zote za jamii..

Kupanga Mbeya ni rahisi sana kuliko.kupanga slums dwellers wa Mwanza ambao 70% ya population wanaishi kwenye mabanda kule milimani..

Mwisho Master plan inalenga kuhakikisha hakuna slums Mpya zinazoibuka..
 
Kwamba hiyo masterplan inahusisha ujenzi wa fremu za kupangisha CBD?
Kwanini halmashauri ya mji wa mbeya inapenda sana Fremu ?
View attachment 2656258
Fremu kujengwa Zina shida gani? Kwamba Leo hii NHC inavunja makazi yake ya zamani huko Dar ,kwani pindi ikojitajika kujenga vinginevyo hizo fremu zitashindwa kuvunjwa?

CBD Wala Haina Uhitaji kama ilivyo Eneo la Kando ya Barabara Kuu ndio maana unaona Kuna shift ya majengo ya biashara.
 
Usipangie watu Maisha,wewe ongea unayotamani yawe vinginevyo pita kushoto..

Mbeya ya Leo is way better than it used to be in 2010 wakati ikitangazwa kuwa Jiji..

Njoo 2025 pia kuandika utopolo wako maana by that time Barabara Kuu njia 4 itakuwa imeisha,Barabara za mitaa km 27 zitakuwa zimeisha na ujenzi wa Stand kubwa za Kisasa utakuwa unaendelea..View attachment 2656232

Njia 6 Kwa Sasa haipo sana sana Kuna mradi wa BRT mbeleni na njia ya Sasa ndio itakuwa reserved Kwa Ajili ya BRT..

Mbeya ipi ambayo watu hawajengi Makazi ya Kisasa? Wewe sema Serikali iongeze Kasi ya kupima Mji..

Kitu pekee nachokuunga mguu ni Chuo Cha Kilimo na JKT hapa Uyole wapishe waende Wilayani hayo maeneo yapimwe na yagawiwe viwanja kama ilivyo Kwa Forest au Iwambi Mpya,hakuna Cha NHC,hao NHC wakajenge Dodoma huko.

Hiyo picha ndo umeona kete muhimu kutetea hoja yako? Bure kabisaaa.!!
 
Master plan ?, eti umesema master Plan ?
Hebu niambie Masterplan itafanya nini na Mbalizi? What will masterplan do with Iwambi na makunguru na Airport ? Uyole? Ilemi?
Ule mji ushakosewa. Hakuna kitu kitafanyika.
Nyumba za kisasa zinajengwa wapi ? Forest mpya na Iwambi?
Elewa , naijua mbeya nje ndani.

Master plan ya Mbeya ni nzuri sana, ila master plan zetu nyingi ni ndoto katika makaratasi.

Hazielezi vyanzo vya fedha za kuwekeza katika kufanya major transformation za miji zitatoka wapi, na wala hazitengenezi mapendekezo ya institutional framework nzuri ya kuwezesha utekelezaji wa master plan.

Master plan hazina enforcement kwenye details level, mfano, nani anamuwajibisha Tanroad kuweka pedestrian provisions wakati wa kudesign na kutekeleza miradi yake, nani anamsaidia Tanroad kuondoa waoegesha magari hovyo na kujiwekea matoleo ya access wanavyojisikia?

Inaishia kusema Area A itakuwa viwanda halafu inamuachia Halmashauri Muandaaji wa mipango kina kusema viwanda vya aina gani vitapangwa kwa namna Gani nk.. hakuna ndoto ya kupokezana vijiti, na ni mpaka tubadilishe Hilo mipango yetu itaanza kuwa useful for now tunachora chora tuu.

Kwa issue ya Mbeya, ni Kijiji kikubwa kama ilivyo DSM vyote ni vijiji vyenye huduma nyingi na occationally wanapatia kitu kimoja katika vingi vinavyofanya iwe. Honestly hizi ni squatters in planned veil.

Haina Order. Na miji inapaswa kuwa na order. Ukikosa order usijiite mji, wewe ni Kijiji tuu.
 
Back
Top Bottom