Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,580
- 9,479
Afisa Mtendaji Kata ya Lusungo, Bw. Edestus Clemence Ndunguru, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kwa shtaka la kuomba na kupokea Rushwa ya TZS 200,000/= ili amsaidie mwananchi kuongea na askari polisi waweze kumpa dhamana katika Kituo cha Polisi Ipinda.
Akisoma shtaka katika kesi hiyo ya Jinai Na. 2946/2024 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Mhe. A. S. Njau na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Wakili Sospeter Tyeah alisema, kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na 11 ya Mwaka 2007
MSHTAKIWA ALIKANA KOSA HILO na alipelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana kwa kutokutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 20, 2024 ambapo mshtakiwa atasomewa hoja za awali(phg)