Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,330
- 4,692
Polisi mkoa Njombe wanamshikilia Israel Msigwa Almaarufu kama "Mtoa Roho"(39)makazi wa Makambako kwa kumsababishia kifo mtoto Haskad Msigwa (7) kwa kumuadhidu kwa nyaya za umeme na fimbo kwa sababu amekojoa kitandani.
RPC wa Njombe Hamis Issah amesema "Huyu amemuadhibu mtoto wake kwa kumuadhibu kwa nyaya za umeme pamoja na fimbo matokeo yake amemsababishia kifo mtoto wake halafu akakimbilia Kilosa Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
"Mzazi huyu alitoweka na alipotoweka tumemkamata jana eneo la Kilosa Mufindi Mjini Mafinga na sasa tunamshikilia lakini mtoto amepoteza maisha, tukikamilisha upelelezi sheria zitafuata mkondo wake. Amesema RPC Issah