Mazoezi na mapishi bora: kabiliana na umri na Saratani

Baba Vladmir

JF-Expert Member
Aug 31, 2021
363
599
Mazoezi ni kitendo cha kuushughulisha mwili kwa muda maalum.

Wakati wa tendo hili , chembe hai huunguza sukari ( glucose) ili kupata nishati(ATP) na mabaki ya sukari.
Mabaki ya sukari baada ya kuiunguza ( AMP) husisimua king'amuzi (exercise sensor) kilichoko kwenye chembe hai. King'amuzi hiki kitaalam huitwa AMPK.
Mazoezi yoyote ya muda mrefu ( endurance exercise) husisimua( activates) king'amuzi hiki.

Nini hutokea unaposisimua king'amuzi cha mazoezi ( AMPK);

Chukua mfano wa king'amuzi cha TV, unapokiwasha huweza kutambua channeli mbalimbali.

Mosi: Usisimuaji wa AMPK huufanya mwili kuwa na uwezo mkubwa wa kuunguza sukari iliyoko kwenye damu(improves insulin sensitivity).Baadhi ya dawa za ugonjwa wa kisukari ( Glitazone) husisimua king'amizi hiki ili kuongeza uwezo wa mwili kuchoma sukari.

Pili:King'amuzi hiki huongeza uwezo wa misuli kutengeneza mashine za kuchoma au kuunguza sukari , mafuta na protein unayokula ili mwili upate nishati. Mashine hii kitaalamu huitwa Mitochondria.
Mazoezi ya masafa mrefu ( endurance exercise) huongeza uwezo wa misuli kutengeneza mitochondria ( PGC 1 alpha activation). Mtu asiyefanya mazoezi hukosa nguvu za kuendelea na mazoezi( exercise intolerance), misuli kushindwa kufanya kazi.

Tatu: King'amuzi cha AMPK huzuia chembe hai kufa kabla ya wakati wake( anti aging) na hivyo kuzuia uzee wa mapema. Kazi hii hutokana na ongezeko la mwili kusafisha taka zake kama chembe ndogo ndogo zinakokufa hivyo kuondoa mrundikano taka unaoweza kuua chembe hai za mwili( increased autophagy and mitophagy)

Nne; Usisimuaji wa AMPK huzima mtambo wa chakula au nutrient sensor ( mToR complex) inayoweza kusababisha saratani ( somo pana lina maelezo yake).
Faida ya mazoezi ya masafa ( endurance) ni pamoja na kupunguza risk za saratani.

UMUHIMU WA KUSISIMUA AMPK KATIKA TIBA:

Baadhi ya dawa husisimua AMPK : Mfano Metformin na Asprin husisimua mashine hii hivyo kuongeza/ kujumuishwa kwenye matibabu ya saratani na hata kwenye dawa za anti aging.
( Note, Metformin ni dawa za kutibu Kisukari na Asprin huyeyusha damu: Usitumie bila mwongozo wa Daktari husika).

MAPISHI BORA : Unapokuwa unafanya mazoezi tumia mafuta ya nazi( MCT) , karanga ( Peanut butter) , olive oil , alizeti , mawese ( Nitawaletea somo).

Punguza matumizi ya vyakula vya kukaangwa , Ongeza vyakula vya Protein hasa samaki mwenye mafuta , Protein za mimea pamoja na matumizi ya vizuia sumu ya mwili ( Mboga zenye ukijani na Matunda)
Nitaendelea na somo la mapishi.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom