Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 19,840
- 21,840
Kwamba sasa mazingira ya kufanya kazi za siasa ni sawa, lakini kuna uhuru wa kufanya siasa bila mipaka, vizuizi wala vipingamizi ilimradi tu kufuata na kuzingatia sheri na kuzitii bila shuruti, kiburi au ukaidi...
Uhuru kwa vyama vya siasa kukusanyika kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara bila kuzuiwa.
uhuru wa kuijieleza na kutoa taarifa au maoni kupitia vyombo vya habari ukilinganisha na kipindi kilichopita...
Uhuru na haki kwa vyama vya siasa kufanya maandamano ya amani na kuwasilisha madai, malalamiko, hoja, mapendekezo na maoni yao kwenye taasisi, idara, mamlaka, mashirika ya kitaifa na kimataifa kadiri waandamanaji wanavyoona inafaa n.k
Uwajibikaji serikali katika kuwatumikia wananchi, uwazi na utawala bora wa Sheria vina tekelezwa kikamilifu licha ya kasoro na dosari kidogo za kibinadamu za hapa na pale...
Mifumo ya utoaji haki na huduma kwa wananchi imeimarika zaidi huku mahitaji muhimu ya wananchi yakitolewa kwa kuzingatia muda, mathalani huko kwenye vyombo vya kutolea haki n.k..
Uhuru wa vyombo vya habari na mazingira bora ya kupata na kutoa habari, yameboreshwa na yana usawa zaidi ukilinganisha na kipindi kipindi kingine na hali hii imepelekea kuibuka au kuanzishwa kwa vyombo vya habari vingi zaidi nchini Tanzania...
Umoja, amani na utulivu pia vimeimarika sana, katika awamu hii ya sita chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan kwasabb ya mazingira bora ya uhuru, haki na usawa katika kufanya siasa miongoni mwa vyama vya siasa na utoaji huduma kwa haki na usawa kwa wananchi...
Kuimarika kwa hali ya kisiasa nchini pia kumechochea huduma za kijamii kama vile maji, afya, elimu, kilimo, miundombinu, uvuvi, usafishaji n.k kuimarisha zaidi..
Hayo ni kwa uchache tu,
ukweli ni kwamba Dr Samia Suluhu Hassan Rais na kipenzi cha waTanzania, amaifungua nchi ni vile tu baadhi ya wanasiasa wa Tanzania wamezoea ukaidi ili kupata huruma ya wananchi wanapotiwa nguvuni kwa kukiuka sheria na kuhatarisha amani kwa kuendekeza siasa za fujo, wanashindwa kuacha kudeka na kukaidi kutii sheria bila shuruti na matokeo yake kwa makusudi wanakutana na mkono wa sheria ili baadae wapate cha kuwaambia wananchi ili waonewe huruma..
Mungu Ibariki Tanzania 🐒