Mazingira: Kila familia Tanzania kumiliki jiko la gesi

RingaRinga

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
1,041
510
Soma nukuu hii
"Katika kuhakikisha Watanzania wanafaidi rasilimali za nchi yao serikali inao uwezo wa huhakikisha kila Mtanzania anamiliki na kutumia jiko la gesi"
Staki kumtaja msemaji wa maneno haya lakini ukweli ni huu:-

Watumiaji wa mkaa wanauwezo mkubwa wa kutumia teknolojia ya gesi kupika, hata hivyo gesi si kitu ambacho Watanzania walio wengi wanakichukulia kuwa kitu chenye umuhimu wa kipekee katika mambo haya ;-

Mazingira:
Ni vigumu kwa Mtanzania mmojammoja kuona kuwa yeye kama mtu mmoja kwa kutumia gesi kupika anakuwa anaokoa mazingira, lakini kama itafanyika kampeni ya kitaifa kuhakikisha kila familia inakuwa na jiko la gesi na elimu ikatolewa naamini Watanzania wengi watahamasika kutumia gesi katika mapishi na wauza mkaa watahamia katika kuuza gesi.

Kazi ya serikali itakayobaki ni kusimamia utunzaji wa mzingira na kuthibiti kwa asilimia isiyo na madhara uchomaji wa mkaa kwa ajili ya matumizi madogo ya lazima kadri itakavyoona inafaa.
Naamini serikali ikiweka utaratibu inaweza hata kama ni kwa mkopo usio na riba.

KUBORESHA MAISHA:
Matumizi ya gesi yanamchango mkubwa kuboresha maisha katika;-
-kuokoa muda
-kubana matumizi
-kuepuka usumbufu na kero
NB: Ni raha tupu kupika kwa kutumia gasi, ni ishara ya kupiga hatua ya ustaarabu na uelewa km si ujanja usio na gharama za ajabu.
Wakati mwingine watu ni wazito tu wa kubadilika lakini wakihamasishwa matumizi ya gesi yataongezeka lakini pia asilimia zaidi ya 90 (ukiacha waoga wa kutumia gesi) wangependa kutumia gesi ili kuboresha maisha yao.

Pia tukumbuke kuwa-
Iwapo serikali italichukulia swala hili kwa umuhimu wa kipekee, ile tafsiri ya wazawa kufaidi rasilimali za nchi yao itakuwa imethibitika vizuri pia.
 
Kumiliki mtungi wa gesi sio ishu, ishu ni kujaza kila inapoisha. Mkaa hauepukiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…