Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,732
- 13,485
Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo akizungumza katika Kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM anasema “Kwenye ulimwengu wa kidijitali wewe ni bidhaa ambayo inatokana na namna ambavyo wewe unachakata maudhui (algorithm).”
Hivi ndivyo mitandao inavyotengeneza pesa, kuna maudhui utayaona unapofungua mitandao lakini hutajua kama ni matangazo na yanaletwa kwako maalum ili uweze kufanya maamuzi mengine.
Dunia ya leo unategemea taarifa ili uweze kufanya maamuzi, iwe taarifa sahihi au potofu, kuna watu wanalipia gharama kubwa Nchi fulani ili wapte taarifa fulani na waweze kufanya maamuzi.
MAXENCE MELO: KILE UNACHOKIPENDA NDICHO UNACHOLETEWA KWENYE DIGITALI
Kwenye ulimwengu wa kidijitali wewe ni bidhaa ambayo inatokana na namna ambavyo wewe unachakata maudhui (algorithm).
Amesema hayo katika Kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM na kuongeza “Hivi ndivyo mitandao inavyotengeneza pesa, kuna maudhui utayaona unapofungua mitandao lakini hutajua kama ni matangazo na yanaletwa kwako maalum ili uweze kufanya maamuzi mengine.
Melo anaeleza kuwa “Dunia ya leo unategemea taarifa ili uweze kufanya maamuzi, iwe taarifa sahihi au potofu, kuna watu wanalipia gharama kubwa Nchi fulani ili wapte taarifa fulani na waweze kufanya maamuzi.”
MAXENCE MELO: BAADHI WANA VIFAA NA HAWAJUI KAMA NI VYA DIGITALI MFANO KUNA AC ZINAZOTUMIA WI-FI
Dunia ya Kidigitali ni pana, Digitali inaanzia katika urahisishaji wa vitu, na haiwezi kuitwa Digitali bila uwepo wa vifaa vinavyotumika na wengine wanavyo lakini hawajui kama ni sehemu ya digitali.
Anaongeza “Kuna baadhi ya nyumba AC zinatumia Wi-Fi na unaweza kuzima hata ukiwa mbali, na ili kurahisisha hilo ndipo hapo matumizi ya internet yanapoingia ili kurahisisha kazi iwe nyepesi ya matumizi ya Digitali."
MAXENCE: HAKUNA MMILIKI WA INTERNET DUNIANI
Kazi ya Internet ni kuunganisha vifaa vya Digitali ili kazi iwe rahisi zaidi, pia watu wengi wanaaminia Serikali inamiliki internet, si kweli bali inaweza kudhibiti miundombinu.
Internet ni uvumbuzi uliotokana na Kijeshi la Marekani wakati likitafuta njia rahisi ya kuwasiliana, baadaye teknolojia hiyo ikatoka jeshini na kuingia katika Ulimwengu wa raia na katika ulimwengu wa internet ni vifaa vyote vinakuwa vimeungana.
SERIKALI INA WAJIBU WA KUWALINDA RAIA HATA MTANDAONI
Kuna wahalifu wengi wameingia kwenye Ulimwengu wa mtandao, wanatafuta mbinu mbadala kadiri Digitali inavyokua.
Digitali ni nzuri sana lakini mamlaka za Nchi zinawajibu wa kuweka mfumo au miongozo na si Sheria ili kulinda watu wake.
KATIBA INAELEKEZA MAMLAKA ZA NCHI KULINDA FARAGHA ZA WATU WAKE
Tangu Mwaka 2020 ameshiriki kutengeneza muongozo wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi ikiwemo Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwenda kwenye kanuni zake mbili pamoja na kufanya utafiti wa Nchi 36 Duniani kisha kutengeneza utaratibu ambao unaweza kufaa kwa Tanzania
Baada ya hapo wakapendekeza Muswada wa Wananchi unaoelekeza nini kifanyike ili faragha zilindwe kama inavyoeleza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 16 kuwa Mamlaka za Nchi zinatakiwa kuweka utaratibu wa kisheria wa kulinda faragha za watu wake
Ulimwengu wa Digitali wananchi wana hatari ya faragha zao kuingiliwa kirahisi kama hakutakuwa na muongozo.
TANZANIA NI KATI YA NCHI ZINAZOFANYA VIZURI AFRIKA KATIKA USALAMA DIGITALI
Naweza kuwatetea kidogo Jeshi la Polisi, kwa sasa wamewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye usalama wa mambo ya Dijitali, Tanzania ni miongoni mwa nchi tano zinazofanya vizuri zaidi barani Afrika kwenye usalama digitali.