Mawazo yangu juu ya elimu yetu

Azpilicueta

Member
Sep 8, 2021
85
100
Habari wakuu
Mwanzo
kwangu msingi wa maendeleo katika jamii ni migongano inayozaa kutokukubaliana au kukubaliana baina ya mtu na nafsi yake, Mtu na Mtu, jamiii kwa jamii au Taifa kwa Taifa migongano hiyo hutokana na huelewa wa mtu juu ya mambo mbalimbali huelewa huja kwa kutengenezwa na kukuzwa ndani ya ubongo wa mtu kwa elimu ya mfumo au njee ya mfumo kwa mtu kujifunza mwenyewe. Hii migongano ndani ya mtu imetupa maendeleo kwenye nishati kama umeme duniani na mambo mengine mengi, migongano kati ya jamii na jamii imetupa uhuru leo yote ni yanaletwa na knowledge iliyozaa migongano ya kutokukubaliana.

Elimu yetu ilipotoka na sasa ni mambo tofauti, kaka yangu amewahi kuniambia yeye alifanya mitihani mitatu yenye jumla ya marks 150 na kwenda sekondari inabidi uwe na 130 hii ni kwasababu ya uhaba wa shule, lakini kuanzia 2010 kuja huku ni quantity iliyonyimwa quality, 2010 marks kuanzia 100/250 walianza kwenda sekondari 2012 tukaletewa ku shade hadi hesabu kuja mbele zaidi hadi Mtoto mwenye 70/250 anapelekwa eneo linaitwa pesh alafu akifaulu uko anajiunga na form two wa mfumo wa necta.

Yani ni kuhakikisha kila alienda shule anafika walau o level bila kuzingatia maarifa yao na uwezo wao, elimu ya o level kuna wakati ilipewa division five yote ni kutafuta mazingira ya quantity iongezeke bila kujali ubora. Zamani ukienda UDSM unakutana na midahalo na mijadala mzito na kweli ukisikiliza unaona ubora wa vichwa vya wanafunzi hao bila kujali wanachobobea.

Kila kitu kinataka kuharibika watoto wana faulu sana yani muhimbili sikuhizi bila one ya tano ubahatishi kwenda, lakini shida si kufaulu shida ni hali mbaya ya wahitimu hawa kuwa weupe kwenye utendaji, huelewa pamoja na maarifa juu ya kazi zao.

Mawazo yangu

Elimu itoke kwenye msingi wa kuogopa kufelisha watu irudi kwenye kuangalia ufikiwaji wa standards, tutazalisha nguvu kazi ya ajabu uko mbele bora namba iwe ndogo ubora uwe mkubwa elimu sio lele mama ukipitia pass marks za vyuo kwenye mataifa ya Japan , korea au iran utaelewa naposema elimu sio lele mama, standards ni muhimu kuwekwa na kuzingatiwa kuliko kujali ufaulu mkubwa. wanafunzi ndio wanapaswa kubadilishwa kwa kupewa mazingira wezeshi ili kuzifikia standards na sio standards kubadilishwa kurahisishia wanafunzi ufaulu.

primary
Hapa me nafikiri kwasababu ya uwepo wa shule nyingi japo azina vifaa na walimu ila atleast zipo, mwanafunzi ili aweze kwenda sekondari anapaswa kuwa na marks 170/250 mitihani ya ku shade iondolewe haifai ina rahisisha tu kazi ya necta kwenye kupunguza muda wa usahishaji , lakini ili kumpa nafasi ya kujiuliza mwanafunzi anapewa nafasi ya kurudia mitihani mala moja ikitokea amehitaji kufanya hivyo.

wanafunzi wanaofeli au watakaokuwa chini ya 170 hadi 100 hawa wanapewa nafasi ya kujiunga na vyuo vya veta, serikali inapaswa kuweka mikakati ya kuwa na vyuo vya veta venye hadhi kama ya veta moshi , DSM au Kama Morogoro katika kila kata ya Taifa hili na hii elimu ya ngazi ya veta inapaswa kuwa funded na kodi zetu watoto wagharimikie gharama zingine sio ada. alkadhalika vyuo hivi vipewe vipaumbele katika kupewa miradi mbali mbali ya serikali ili kuvipa nguvu kujitanua katika mafunzo ya kuendana na kasi ya teknolojia.

wanafunzi wanaobaki wanapaswa wasiwepo kabisaa haiwezekani mwanafunzi akakaaa miaka saba shuleni na akashindwa kufikia marks 100 /250 hawa wanaletwa na mazingira mabovu ya elimu yetu wingi wa wanafunzi darasan pamoja na upungufu wa walimu hili ni swala la serikali kuboresha mazingira ili kila mwanafunzi afikie standards

Secondary
katika ngazi hii masomo yasipunguzwe uelewa unajengwa kwa kusoma mambo mbali mbali, lakini ufaulu kwenda form six iweni kuanzia daraja la pili sio kwa msichana au mvulana wote wasimamiwe na standard moja. wanaoshindwa kufikia hapo wanapata nafasi ya kwenda vyuo kati kwa pass mark ya Kama ilivyo tu sasa.

Ngazi ya advance
Hapa kwa masomo ya science nafikiri panapaswa kuangaliwa mazingira yawe mazuri kuhakikisha practicals ndio iwe msingi wa elimu hii na sio mavitabu mengi yenye mamilion ya nots watu tunashindana kutolala na kumeza huku application hasa ya tulichomeza hatuna na hatujui wala hatuwezi ku apply . walau mtu wa PCM aweze kufanya wiring mwenyewe, vitu kama powerbanks, switch, bulb , redio ndogo waweze kuunda na kuelewa namna ya ku apply theoretical view kwenye maeneo hayo, na kozi tofauti na science zinabidi zipunguzwe kadiri itakavyofaa.

Elimu ngazi ya vyuo vikuu

Huku pamechoka serikali aipahudumii imepasusa pamedumaa kwasabbu ya kukosa matunzo kutoka kwa baba yao serikali, wafanyakazi wachache wataalamu wachache, TCU wapo ila nao ni kama awapo vyuo vimekuwa dhaifu sana.

mwanafunzi anasoma preparation week past papers na anafaulu , mwanafunzi wa chuo kikuu anaulizwa what is ? matching items? maswali yanarudiwa kama necta .
Budget zetu ndogo na ufisadi wa kingono na fedha umefanya mazingira ya vyuo vetu yanakuwa sio ya kumwandaa mtaalamu. vyuo havina ubora kozi ina wanafunzi 200+ mahabara moja tena imechoka.

Nafikrii hapa panapaswa kuwekewa standards juu ya mitihani inavyopaswa kuulizwa kwa kila kozi theory kwa practical Taifa zima, na inspection ifanyike regularly. Lakini hayo yote hayawezekani bila serikali kuboresha mazingira.

Mwisho
Mzazi pambana na mwanao kuhakikisha anapata huelewa kwenye maeneo mbali mbali katika ukuaji wake kama kinanda kipo karibu mpeleke ajifunze , kama una ujuzi wa ujenzi, electronics, chochote muambukize na mwanao hakikisha anakuwa na ujuzi elimu yetu haitampa hayo na maisha yanataka hayo, pambana na wanao wapate skills na knowledge ndio msingi wa maisha yake na kujitegemea kwake.Asante
 
huwezi kusoma kitu ambacho hakina uhusiano na MAISHA yako halisi ukasema umepata Elimu

Watu wengi smart huwa wanafikia hatua ya kuwa na maarifa Kwa kujijengea utamadunia Wa Kusoma vitabu kutoka sehemu tofauti tofauti.
 
tufanyaje kizazi hichi em njoo huku mburahati uone ao watoto wa sekondari
 
Ukitaka kufanikiwa jikomboe wewe kwanza ,ukifanikiwa kujikomboa ndo uanze kuwaza kuwakomboa watu wengine.

Mzazi anazaa mtoto ambaye hana uwezo wa kumpa malezi bora wala Elimu bora.

Suluhisho na kuhakikisha unapambanaia kizazi chako Kwa kukipa Elimu bora na malezi bora
PESA au ajira nzuri hutokana na MTU kuwa marketable in positive thinking
 
Back
Top Bottom