Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 122
- 210
Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Filamu ya China zinaonesha kuwa hadi kufikia Februari 3, mauzo ya tiketi za filamu katika kipindi cha sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2025 yamefikia yuan bilioni 8.02 na kuweka rekodi mpya ya kihistoria.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, filamu ya katuni ya “Ne Zha 2” imeingiza yuan bilioni 3.8, ikifuatiwa na filamu ya "Detective Chinatown 1900” iliyoingiza yuan bilioni 1.98, huku filamu ya "Creation of the Gods II: Demon Force" ikichukua nafasi ya tatu kwa kuingiza pato la yuan milioni 933.
Mauzo ya jumla ya tiketi za filamu nchini China kwa mwaka 2025 yamefikia yuan bilioni 9.82, yakipiku yale ya Amerika ya Kaskazini na kuchukua nafasi ya kwanza duniani.