peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,942
Kifo cha utata cha Aron Mfugale, mwanafunzi wa kidato cha sita, Shule ya Sekondari ya Mawelewele iliyopo Iringa kimekuwa sehemu ya matukio ya mauaji ya kutisha yaliyotokea ndani ya wiki moja katika mikoa mbalimbali nchini na kuacha simanzi kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Mbali na kifo hicho, matukio mengine ni ya jijini Mwanza, likiwemo la mume kudaiwa kumuua mkewe, mvuvi kutuhumiwa kumuua mwenzake wakigombania samaki huku mwingine akishikiliwa kwa tuhuma za kumtoa kafara mtoto wake kwa kumfukia ardhini akiwa hai ili apate mali.
Kana kwamba hayo hayatoshi, mkoani Rukwa, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kasanga iliyopo Kalambo, Michael Royan (31) anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu katika nyumba ya kulala wageni iliyopo mjini Sumbawanga.
Nini kimempata Kelvin?
Kwa mujibu wa Aron Mfugale, baba mzazi wa mwanafunzi huyo, Kelvin alifariki Novemba 19, mwaka huu akiwa katika mazingira ya kutatanisha shuleni.
“Ilikuwa saa mbili asubuhi, nilipopigiwa simu na mwalimu akajitambulisha na kuniambia moja kwa moja kuwa ‘nakutaarifu Kelvin Mfugale amefariki’, nilihamaki na nikakata simu nikihisi hao ni matapeli,” alisema Mfugale.
Habari zilizolifikia Mwananchi ni kwamba Kelvin alipoteza maisha baada ya kupigwa na wanafunzi wenzake katika maeneo ya shule, akituhumiwa kuwataja kwa kumiliki simu shuleni kinyume cha taratibu.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Sunday Songwe alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuwa wanafunzi watatu wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kusababisha mauaji hayo.
“Ni kweli tukio lipo na tunaendelea na upelelezi. Baba yake mzazi aliripoti na tuliruhusu ifanyike ‘post mortem’ na ripoti ya daktari inaonyesha ubongo wake ulivilia damu,” alisema Kaimu Kamanda na kwamba upelekezi unaendelea.
Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Tupe Kayinga alisema tukio hilo lipo chini ya polisi kwa ajili ya upelelezi.
“Ni kweli taarifa ya kifo cha mwanafunzi wa kidato cha sita ipo na ilipelekwa kituo cha polisi na sasa wanaendelea na uchunguzi,” alisema Kayinga.
Mwili wa mwanafunzi huyo ulizikwa katika Kijiji cha Ivavi, Ifunda Wilayani Iringa, karibu na kaburi la baba yake mkubwa, Patrick Mfugale, aliyewahi kuwa mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).
Simulizi ya kifo
Akisimulia mazingira ya kifo hicho, Aron alisema kabla ya kifo cha mwanaye, alirejea nyumbani akidaiwa kupatikana na makosa mawili -- kumiliki simu na kuchoma godoro la mwenzake.
Alisema Novemba 17, mwaka huu aliongozana na mwanaye hadi shuleni kuomba aendelee na masomo.
Alisema baada ya kufika akaelezwa makosa hayo na kuwa mwanaye alitakiwa kupewa adhabu ya kusimamishwa shule au baba yake alipe matofali 3,000 kwa kila kosa.
“Lakini mtoto alilikataa kosa la pili la kuchoma godoro... Niliwaambia hata nyumba yangu ninayoishi sijawahi kujenga kwa tofari hizo na mimi natamani mtoto aendelee kusoma. Baada ya majadiliano wakanipunguzia hadi tofari 3,000 na mifuko mitano ya smenti.”
Alisema baada ya kuandika maelezo akiahidi kulipa ndani ya siku saba aliondoka akirejea nyumbani akimwacha Kelvin salama shuleni.
Ilipofika Jumamosi asubuhi alipokea simu kutoka kwa mwalimu akimtaarifu kuwa mwanaye amefariki dunia.
“Nilikata simu, akapiga tena na kuniuliza mbona unakata simu? Akasema taarifa ndiyo hiyo ni kweli Kelvin amefariki. Akili yangu ilikuwa haijakaa sawa, nikaenda kumwambia mdogo wangu Wilbert ambaye pia alibaki anashangaa,” alisema Mfugale.
Wilbert alisema alilazimika kupiga simu shuleni naye alielezwa taarifa za kifo hicho.
Alisema walianza mpango wa kwenda shuleni kujua ukweli, lakini baada ya kufika mjini na kuwasiliana na shule, waliamua kukutana Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kuona mwili na kubaini ni kweli.
“Tulipoona mtoto ni mwenyewe tukatoka nje, wakatuuliza mazishi lini? Tukashangaa mbona haraka? Tulitoka tukachukua jukumu na kwa sababu tulikuwa na hofu ya kifo cha mtoto, tuliamua kwenda polisi kutoa taarifa,” alisema Wilbert.
“Kiukweli hakukuwa na taarifa za kueleweka za kifo cha mtoto, tukaanza kuhangaika kujua ukweli, ndipo tukawaomba polisi watusaidie uchunguzi wa kidaktari, kinachosikitisha mtoto baada ya kupigwa alibebwa na wenzake mpaka hospitali,” alisema Wilbert.
Kwa mujibu wa wazazi wa Kelvin, inasemekana kijana huyo aliingia katika ugomvi na wenzake baada ya kuwataja katika mahojiano na uongozi, kuwa na wao wanamiliki simu.
Aron alisema anachoomba ni haki itendeke japo ameshampoteza mwanaye.
Kuzikwa kwa kafara
Mkoani Mwanza, Jeshi la Polisi linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Mahaha, wilayani Magu, Zawadi Msagaja (20) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kike kwa kumfukia ardhini akiwa ni kafara ya kupata mali.
Wengine wanaoshikiliwa katika tukio hilo ni Elizabeth Kaswa (dada yake Zawadi) na shemeji yake (mume wa Zawadi), Mussa Mazuri ambaye ni mganga wa kienyeji aliyetoa maagizo ya kutekelezwa kwa kitendo hicho, huku akimtishia Zawadi kuwa asipofanya hivyo, yeye ndiye atatolewa kafara.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa alisema watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda kitendo hicho Novemba 13, mwaka huu katika Mtaa wa Kisundi wilayani Ilemela.
Alisema mwanamke huyo baada ya kukwepa kutolewa kafara aliridhia kumtoa mwanaye ambapo walimpatia mtoto huyo dawa za kienyeji zilizomfanya akose nguvu, ilipofika saa 2 usiku walimzika akiwa hai shambani katika eneo wanapoishi.
Alisema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema, polisi walimkamata mama wa mtoto huyo na dada yake na baadaye mganga huyo aliyekuwa amejificha Nyanguge.
Alisema mwili wa mtoto ulipelekwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando kusubiri uchunguzi na upelelezi wa shauri hili unakamilishwa ili watuhumiwa wafikishiwe mahakamani.
Adaiwa kumuua mkewe
Katika hatua nyingine, Mutafungwa alisema jeshi hilo linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Bujingwa wilayani Kwimba, Nyanda Thomas (22) kwa tuhuma za kumuua mke wake, Kahabi Kazimili (22) kwa kumchoma na kisu chini ya kidevu.
Mutafungwa alisema uchunguzi unaonyesha mauaji hayo yalisababishwa na wivu wa mapenzi na kuwa Nyanda alikuwa anamtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine.
“Mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alitokomea kusikojulikana, lakini Novemba 21, 2022 alikamatwa akiwa mafichoni mkoani Kagera na kurejeshwa Kwimba kwa hatua za kisheria dhidi yake,” alisema
Ugomvi wa samaki
Jeshi hilo pia, linamshikilia mvuvi wa Kisiwa cha Nyamango kata ya Bulyaheke wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Mnanka Paul (44) kwa tuhuma za kumuua mvuvi mwenzake, Shabani Ally (24) wakigombea samaki.
“Walikuwa wanavua samaki pamoja, baadaye walipata samaki mkubwa, ndipo mtuhumiwa alipotaka kumdhulumu mwenzake, ukazuka ugomvi uliopelekea marehemu apate majeraha na kufariki Novemba 21 mwaka huu akipatiwa matibabu katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema,” alisema Mutafungwa.
Hakimu adaiwa kujiua gesti
Katika mfululizo wa mauaji hayo, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Michael Royan (31) anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Sumbawanga.
Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 27 katika nyumba ya wageni alikolala.
Alisema asubuhi ya siku hiyo ofisa upelelezi wa mkoa wa Rukwa alipigiwa simu na mmiliki wa nyumba hiyo na kueleza kuna mteja ambaye amelala na hajaamka na inaonekana amepoteza fahamu.
Mallya alisema baada ya polisi kufika eneo hilo waliingia ndani ya chumba hicho na kumchukua mtu huyo kisha kumpeleka hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Sumbawanga na baada ya uchunguzi ilibainika mtu huyo amefariki dunia.
Katika uchunguzi wa tukio hilo, alisema walibaini marehemu alikuwa ni mtumishi wa Serikali katika idara ya mahakama na kituo chake kilikuwa ni Mahakama ya Mwanzo Kasanga.
Uchunguzi wa awali alisema unaonesha huenda alikunywa sumu.
Mwananchi