Mauaji ya kiroho Kenya, Tanzania tuko hatarini

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
17,005
20,421
Tukio la tapeli wa kiroho Bwana Paul Mackenzie kuratibu mauaji ya watu zaidi ya 76 kwasasa, ambapo kwamjibu wa makadirio wa Idara ya upelelezi na maafa ya Kenya inasema wanaweza kufika 150 baadae. Kwanadharia ya kijasusi tukio hili ni Uzembe mkubwa wa idara ya Ujasusi Kenya, halina neno unaloweza kulitumia zaidi ya kusema ni Uzembe wa vyombo vya ulinzi na Usalama Kenya. Ni Kenya hiyohiyo yuko mgonjwa wa akili anajiita Mungu kwa sasa na amejaza wafuasi wanaomwamini. Lakini litufumbue kama taifa kurejea kwenye ushauri nilioutoa katika Kitabu cha Ujasusi kuhusu wajibu wa Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS). Kwenye kitabu nimeandika mengi, Kwaufupi nilisema kwamba:

Watu wakiona makanisa ya kikristu yakishamiri au wakiona misikiti na ibada za kiislamu zikishamiri, wasidhani ni kukua kwa imani flani katika nchi, bali ni uimara au udhaifu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Moja ya jukumu la vyombo vya ujasusi ulimwenguni ni kudhibiti na kuongoza mwenendo wa kiroho katika nchi, Nchi isiyotazama mambo ya kiimani kama nyenzo muhimu ya kiusalama, nchi hiyo iko hatarini.

Ukifika Moscow moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Urusi ni kudhibiti miitikio ya kimani katika nchi, na dini kuu ya Othodoksi inadhibitiwa kwa 100% na Shirika la Ujasusi la Urusi la FSB. Vivyo hivyo ukifika London, moja ya wajibu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza la MI5 na hata MI6 ni kudhibiti miitikio ya kiroho, Dini kuu ya London ya Church of England (Anglican) hudhibitiwa na dola moja kwa moja. Rwanda jirani zetu tu hapo napo wameweka moazo na masharti magumu ya kutaka kubudu uholela. Lakini Tanzania, Kenya na Uganga ndiko kuna uholela wa kiimani, kila mhuni akilala na kuamka akisoma mstari mmoja wa bibli anafungua kijiwe na kutangaza ni Mchungaji/Nabii mara Kuhani ama anavuka zaidi na kujita Mungu.

Tanzania kama lilivyo taifa la wajinga, limejaza matapeli wa kiroho kila kona ya nchi hasa kwa dini ya kikristu, Kila ukitembea hatus kumi kuna kijiwe kinaitwa kanisa la mhuni flani, Ni Tanzania hiihii haijasahau mauaji ya juzi tu ya mmoja ya matapeli wa kiroho Boniface Mwamposa aliyewaua watu zaidi ya 30 tarehe 1 February 2020 kwamtindo aliouita kukanyaga mafuta. Huu ulikuwa ni uzembe mkubwa wa idara ya Usalama wa Taifa uliozaa maafa hayo, na badala yake alizawadiwa pongezi na heshima za kitaifa mbele ya utawala wa awamu ile. Lakini Tanzania hapahapa miaka ya nyuma kidogo 2003, kuna mhuni aliyekuwa kachoka maisha, aliwakusanya mamia ya watu, akawapeleka katika pori moja kule Segerea Ukonga akawashindisha njaa, kisha akawasomba hadi uwanja wa ndege, wakiwa hawana hati yoyote ya kusafiria wala nauli, wakaanza kulazimisha kutaka wapande ndege waende Iraq kuhubiri injili, kipindi hicho Iraq ilikuwa imevamiwa na Marekani. Polisi waliwazua, wakarudi kulekule pori la segerea, walikaa miezi kadhaa, njaa iliwachapa wakaanza kuondoka mmojammoja na wengine wakaanza kuwa vibaka na makahaba.

Uzembe wa Idara za Usalama katika nchi ya jirani ya Uganda uliendelea,Miaka ya nyuma kidogo nchini Uganda kwasababu tu ya uzembe wa idara ya Usalama ya Uganda, yuko kichaa mmoja aliyeitwa Joseph Kibweteere aliyezaliwa 16 Novemba 1932 na kutoweka 17 Machi 2000 hadi leo. Joseph Kibweteere alikuwa Mchungaji kiongozi wa Vuguvugu la Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu, kundi ambalo lilijitenga na Kanisa Katoliki nchini Uganda. Umaarufu wake uliibuka baada ya mwaka 2000 kuwachoma moto waumini wake 778 hadi kufa kabisa akiwaaminisha kuwa mwaka huo ni mwisho wa dunia.

Pengine nieleze jambo moja muhimu sana la kidini, Duniani ya Magharibi na Mashariki ya Kati, kuna dini kuu tatu zilizo katika maandishi ya kumbukumbu, ambazo ni Uyahudi, Ukristu, na Uislamu. Kisha kuna mnyumbuliko wa madhehebu kadhaa wa kadhaa, Lakini pia kuna dunia ya Mashariki ya mbali na Urusi, wao nao wa dini zao za Othodoksi na Hindu na Uchina pia. Dunia ya Ujamaa ina dini zao, na dunia ya ubepari nayo ina dini zao. Afrika hatuko kwenye hayo sisi ni fuata upepo tu tumepokea dini za majahazi ndizo hizi zinatusumbua tunauana na matapeli wanazitumia kujipatia utajiri kwa kigeni cha uhuru wa kuabudu.

Dini ya Uyahudi ambayo ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, inayodhibitiwa na Shirika la Ujasusi la Israel la MOSSAD kwa viwango vyote. Uyahudi pia jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu. Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara. Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao. Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo. Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu. Siku hizi wako karibu milioni 21 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Maoni yangu, Tufanye marekebisho ya kikatiba pale panaposema kila mtu ana uhuru wa kuabudu imani apendayo, tuongeze kuwa imani hiyo ipimwe kwanza na vyombo vya kusimania usajili wa makanisa nk. Kubwa zaidi tuzuie mtu kusajili kanisa binafsi. Kanisa kiwe chombo cha umma sio mtu binafsi. Kama ni chombo cha umma maana yake kikaguliwa mapato na matumizi na mamlaka za umma. Tuweke marufuku wa bidhaa yoyote kuuzwa kanisani iwe maji, vitambaa, Mafuta nk vyote hivi ili viuzwe, lazima vitambuliwe na TRA, na vilipiwe kodi. Kufanya hivyo tutazuia utitiri wa makanisa hatari ya wajasiliamali waliojazana kutapeli watu na kujitajirisha huku umma uliojaa kanisani ukiendelea kuwa masikini, kisha wachungaji wanawaambia waumini wenye misongo ya mawazo ati wanamapepo.

Na Yericko Nyerere
 
Kwenye Bandiko lako ONDOA UISLAM, USIWEKE UISLAM kwenye UPUMBAVU wenu. Jikemeeni wajinga wenyewe
Mkuu mbona kamarada Yericko ameongelea tu maslahi mapana ya nchi bora ambayo ndani yake wako watu wa imani tofauti na wote wanahitaji utulivu na AMANI yetu iendelee!!!

Mjadala ni mzuri....wa kujenga na si kubomoa....

Ubarikiwe mkuu ,amin

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona kamarada Yericko ameongelea tu maslahi mapana ya nchi bora ambayo ndani yake wako watu wa imani tofauti na wote wanahitaji utulivu na AMANI yetu iendelee?!!!

Mjadala ni mzuri....wa kujenga na si kubomoa....

Ubarikiwe mkuu ,amin
Ushawahi ona waislam wana huo upumbavu? Ushawahi sikia msikiti wa shekhe fulani?

Mnapotoa mada zenu msitake kubalance story, Uislam hauna huo upumbavu, always ni WAKRISTO ndio wanaaminishwa upumbavu.

Muslims always wanaamini kwa Mungu Mmoja (ALLAH S.W).

Hii mada isichanganywe na UISLAM.
 
Kuna mjinga Mmoja anadai eti hata akiwa shoga hivyo ndivyo mungu ametaka awe ..na nimhubiri sijui nabii eee jamani ukristo umekuwa kituko..sema hatusomi vitabu wandishi wengi wameongelea utapeli wa viongozi wa dini,mfano mzuri ni Wole Soyinka ktk tamthilia "The Trials of Brother Jero"mhusika mkuu Jeroboam (brother Jero) anawaita waumini wake kwa Siri eti my costumers, wateja wake.ni wakati Sasa serikali kuhakikisha Kila anaefungua kanisa awe ni vigezo ikiwemo elimu ya chuo kikuu ili kudhibiti hawa wahuni
 
Ushawahi ona waislam wana huo upumbavu? Ushawahi sikia msikiti wa shekhe fulani?

Mnapotoa mada zenu msitake kubalance story, Uislam hauna huo upumbavu, always ni WAKRISTO ndio wanaaminishwa upumbavu.

Muslims always wanaamini kwa Mungu Mmoja (ALLAH S.W).

Hii mada isichanganywe na UISLAM.
Akhy relax....

Narudia tena...sidhani kama Yericko ameshambulia wanadini wote....na sidhani pia wewe unaamini kuwa ni "wakristo wote" ndio wako hivyo....kama sivyo basi utakuwa na fikra za "attacking others,prejudice,argumentum ad hominem and generalization" ndani ya bandiko hili la kujenga taifa bora zaidi.......

#SiempreJMT
 
Akhy relax....

Narudia tena...sidhani kama Yericko ameshambulia wanadini wote....na sidhani pia wewe unaamini kuwa ni "wakristo wote" ndio wako hivyo....kama sivyo basi utakuwa na fikra za "attacking others,prejudice,argumentum ad hominem and generalization" ndani ya bandiko hili la kujenga taifa bora zaidi.......

#SiempreJMT
"NINYI MNA DINI YENU NA SISI TUNA DINI YETU".

Kama wa moto awe moto sio wavuguvugu, hii mada haikupaswa kuingizwa hata neno Uislam.

Miaka mingi sana, sisi tulikemea haya makanisa yasiyo na mbele wala nyumba hasa matapeli kutoka MBEYA, IRINGA, ARUSHA hayo maeneo yana wapumbavu wengi sana.
 
"NINYI MNA DINI YENU NA SISI TUNA DINI YETU".

Kama wa moto awe moto sio wavuguvugu, hii mada haikupaswa kuingizwa hata neno Uislam.

Miaka mingi sana, sisi tulikemea haya makanisa yasiyo na mbele wala nyumba hasa matapeli kutoka MBEYA, IRINGA, ARUSHA hayo maeneo yana wapumbavu wengi sana.
Kwani umesahau vijana wanaenda wanaovaa mabomu nakwenda kujilipua ili wafe wakapewe bikra 72? Na vijana wakitanzania waliokuwa wanaenda kujiunga na Al shabab Kuna mmoja alikamatwa Kenya kwenye ya mauji ya pasaka huko garisa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushawahi ona waislam wana huo upumbavu? Ushawahi sikia msikiti wa shekhe fulani?

Mnapotoa mada zenu msitake kubalance story, Uislam hauna huo upumbavu, always ni WAKRISTO ndio wanaaminishwa upumbavu.

Muslims always wanaamini kwa Mungu Mmoja (ALLAH S.W).

Hii mada isichanganywe na UISLAM.
Ila kumpiga shetani kwa kumrushia mawe wewe ndio unaona hizo ni akili?
 
UZI BORA WA MWAKA.

HII INAONYESHA TISS KUWA DHAIFU NA SABABU KUU NI NAMNA YA KU-RECRUIT HAO VIJANA.

TISS MKO WAPI KATIKA UJASUSI WA KIUCHUMI,UJASUSI WA KIDINI,


KAMA MNAPIGA KAZI KAMA ILIVYO KADA YENU KIMYAKIMYA ILA KWENYE SWALA LA DINI MMEFELI

KUNA TAPELI MMOJA ANASEMA ETI WAENDE NA KUCHA NA NYWELE WAOMBEWE

SHIT
 
Kuna mjinga Mmoja anadai eti hata akiwa shoga hivyo ndivyo mungu ametaka awe ..na nimhubiri sijui nabii eee jamani ukristo umekuwa kituko..sema hatusomi vitabu wandishi wengi wameongelea utapeli wa viongozi wa dini,mfano mzuri ni Wole Soyinka ktk tamthilia "The Trials of Brother Jero"mhusika mkuu Jeroboam (brother Jero) anawaita waumini wake kwa Siri eti my costumers, wateja wake.ni wakati Sasa serikali kuhakikisha Kila anaefungua kanisa awe ni vigezo ikiwemo elimu ya chuo kikuu ili kudhibiti hawa wahuni

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
Elimu ya chuo kikuu haitoshi, waongeze na ukubwa wa eneo la kujenga hilo kanisa, kwa sasa kila mtaa kuna kanisa, kama kukiwepo sharti ukubwa wa eneo kujenga kanisa nadhani ingesaidia, masharti yawe magumu kama ya kuanzisha shule, hospital, zahanati.
 
Hata useme bado wajinga watasahau na kesho wakisikia mwamposa ana mafuta mapya watalundikana kukanyagana tena.
Hapo sasa ndipo lawama zote kwa TISS na mamlaka. Hivi kweli mpumbavu mmoja anayejiita yesu wa tongareni sijui anaweza kuachwa na mamlaka kufanya upumbavu ulie? Kesho wakiskia amewazika watu kadhaa baada ya kuwaua tutashangaa nini.
 
Kwa Jiji la Mbeya hii ni aibu sana sana!kila kona kuna kanisa na mengine hayana usajili na Mamlaka zipo!

Mbunge wa Iringa jana kaongea Bungeni kuwa watu wetu hawana afya ya akili "utakuta Mama ndani ya pochi lake kabeba maji ya upako,chumvi ya baraka,mara kitambaa cha bahati..." Hizi ni dalili za watanzania wengi hawana afya ya akili,Jesca Mtavambangu Mbunge wa Iringa anasema!

Wakati haya yanatokea Mtume Mwamposa pale Mbeya maeneo ya Ifisi kama unaelekea Songwe Airport kajenga Bonge la Hotel yake binafsi!Wizi huu kwa masikini haukubaliki!

Naunga mkono hoja sana!
 
Back
Top Bottom