kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,567
- 23,034
Aliyekukariririsha istilahi weledi kaleta dhahama jamvini. Nilcho kiona ni kulitaja neno weledi na kutaja lawama. Hukusema matendo yapi ya kiuweledi yaliyotakiwa kufanywa. Unachojua na ndicho ulifundishwa na walimu wako ni kulaumu tu. Hujajaliwa wala kufunzwa kushauri.Kwanza nikupe pole IGP na nijipe pole kama raia kwa kupoteza walinzi wetu wa usalama wa raia,bila ya wao kusimamia usalama wetu saa hizi hali ingekuwa mbaya zaidi,
Dhumuni langu ni kuwa jeshi la polisi halifanyi kazi zake katika kiwango cha juu ila ni zimamoto polisi wetu hutumika vibaya tu pindi panapotokea matatizo ya vyama vya siasa na kukabili mtu mmoja mmoja kwa maslahi ya mtu aliewatuma
Sitaki kusema tukio hili ni la kisiasa sababu tusigeuze siasa ni dampo la kutupia kila baya
Jeshi la polisi tanzania hufanya shughuli zake kwa matukio ya muda mfupi mfano wiki hii pametokea ujambazi mwananyamala basi polis watakurupuka na kuvamia mwananyala na kubeba watu wa kata nzima na mwisho wa siku watatafuta chaka huko mbezi watulitee maigizo kuwa wamekamata silaha za kivita pesa,mapanga,pinde na mishale eti kuwa hilo ni chimbo la majambazi
Baada ya hapo wale watu wa mwananyamala wataachwa wakiozea magerezani bila kutendewa haki na waliokamatwa si wahusika na kesi wamebambikiwa bado hiyo haijakuwa na uhasama kwa polisi na jamaa za wale mliowapoteza magerezani kwa kuwaonea
kwanini msimkate mtu mkamuhoji mkihisi hausiki mumuachie lakini wakati huo ukimfuatlia kwa ukaribu lakini polisi wakishatia kijiji ndani wao ndio wameshamaliza hakuna ufuatiliaji
sasa kwa hili linalojiri sasa ni matokeo ya uvivu wa kutofuatilia mambo kwa muda mrefu eneo hilo mlikamata silaha na pesa mkasema ndio waliovamia kituo cha stakishari baada ya hapo ameuwawa mkuu wa polisi akafuata kiongozi wa ccm sasa ni polisi na ndani ya hapo mmeshakamata watu wengi sana bila ya kuwa na uhakika
Na tunajua jeshi la polis linapohoji watuhumiwa hutumia nguvu je bado hamjatengeneza uhasama na raia na ndio wameshaanza hivyo moja jumlisha mbili ni tatu bila kufanya kazi kwa uweledi mambo hayo hayatakoma na yatasambaa nchi nzima
Polisi angalieni utendaji wenu sio kuonea watu na kuwambikia kesi!
IGP waongezeeni askari silaha ikiwa wapo kumi kuwe na silaha kumi sio watu kwenye difenda moja wapo patrol askari kumi bundiki mbili huo ni udhaifu mwingine tujikinge kabla ya hatari!
Aksanteni
Kazi hiyo nimekuachia wewe mwalimu wa chuki!Aliyekukariririsha istilahi weledi kaleta dhahama jamvini. Nilcho kiona ni kulitaja neno weledi na kutaja lawama. Hukusema matendo yapi ya kiuweledi yaliyotakiwa kufanywa. Unachojua na ndicho ulifundishwa na walimu wako ni kulaumu tu. Hujajaliwa wala kufunzwa kushauri.
Wewe ni mmoja lakini wapo wengi yaliowakuta ya kusulubiwa na polisi!Dah hii ni kweli, polisi ifanye kazi kwa weledi sasa mimi ni muhanga wa kukurupuka kwa polisi mjomba aligombana na mtu mwingine polisi walivyo mkosa wakaja kunibeba mimi full vipigo na pingu mtaani watu wanashangaa huyu kafanya nini , kumbe ni jambazi nakumbuka mpaka sasa huwa najawa na hasira sana jinsi walivyo nizalilisha
Huko marekani hufanya kazi kwa haki na hapa kwetu hatufurahi yanayotokea isipokuwa ni polisi kufanya kazi kwa haki na kutoacha makovu na visasai katika jamii!Pamoja na kulinanga na kulikebehi Jeshi la Polisi tambueni pia Weledi, Mbinu,ujanja na umahiri wa Magaidi Dunia nzima ni wa kiwango kisichomithilika.
Marekani mpaka Leo inahangaika nao lakin bado wakiingia kwny 18 inawabutua hata ndani ya Marekani.
Raia wa Mkoa wa Pwani wasipobadilika kutoa ushirikiano hili Tatizo halitaisha.
Tunaweza tusione tatizo sana kwa kuwa wanaouawa ni Askari lakin kesho wanaweza kuvamia Makanisa au Misikiti na kuua ili tu kuchonganisha jamii na hili ndio lengo Lao kuu
Huenda wewe ni askari na huwa una tabia ya kubambikia watu kesi na kuwakamata ovyo ovyo , sasa umeguswa na jamaa hapo juu, na pia utakuwa unapenda magendo. Unaungana na majambazi kuwaibia RAIA Mali zao kama akina Abdalah Zombe na wenzake walio waua wafanya biashara wa madini mwaka 2006 kisha kuwa bambikia kesi ya ujambazi. Na hisi na hao wenzio wa mkuranga wamezurumiana mgao na hayo majambazi baada ya kuiba kwa RAIA au taasisi Fulani kisha majambazi yakawageuka na kuwasubiri wakitoka lindo kisha kuwa ua. Fanyeni kazi kwa weledi na si kugeuka na kuwa sehemu ya wahalifu Mtakufa kama nzige nyie.Aliyekukariririsha istilahi weledi kaleta dhahama jamvini. Nilcho kiona ni kulitaja neno weledi na kutaja lawama. Hukusema matendo yapi ya kiuweledi yaliyotakiwa kufanywa. Unachojua na ndicho ulifundishwa na walimu wako ni kulaumu tu. Hujajaliwa wala kufunzwa kushauri.
Wameingia vipi kwenye siasa?Polisi wakiambiwa wakae mbali na siasa huwa wanaona kama tunawaonea gere sana.... Ukweli ni kwamba majeshi yaliyoingia katika siasa yaliisha kwa kovu la aibu hakuna chombo ch ulinzi kinachoingia kwenye siasa kikapendwa na wananchi au raia
Wameingia vipi kwenye siasa?
Wengi bado hamjielewi
Unalaumu polisi ilihali wanasiasa wetu ndo chanzo cha yote, kazi ya askari ni kazi ya orders.
Ukiona polisi kakukamata usijae hasira unapaswa kufikiria nje ya box kwanza.
Duniani kote askari ni watu wa kutii amri(orders) na askari anayekataa kutii amri ya mkubwa wake(eg rais, RC au DC) kiufupi ana adhibiwa kinidhamu ni pamoja na kufukuzwa kazi, sasa akifukuzwa atakuja kula kwako?
Na askari anayekaidi amri halali simply ni msaliti/anapanga kuhaini/anapanga kupindua serikali etc.
Think outside the box
Kazi ya uaskari ni ngumu sana, tunachotakiwa kupata ni wanasiasa makini, mihimili makini kama Bunge na Mahakama.
Siku ukitambua umuhimu wa mihimili hiyo hutakaa uwalaumu askari hata 1%