Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 16,221
- 34,265
Congo DRC ikiwa kwenye hatihati ya kutekwa na Rwanda na Uganda, Wanawake wawili Diaspora wanaibuka na kuisadia nchi yao kuishawishi Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua stahiki dhidi ya Rwanda.
Sote tunafahamu namna Kagame alivyowekeza katika suala la Uhusiano wa Kimataifa.
Sote tunafahamu namna Kagame alivyofanikiwa kutengeneza picha chanya Kimataifa kuhusu nchi yake.
Kagame alifanya hayo kwa makusudi huku akiendelea kunufaika na kutotulia kwa Congo Mashariki.
Kazi kubwa iliyofanywa na Mawaziri Wawili wa Congo ambao ni wana Diaspora, Judith Suminwa Tuluka (Waziri Mkuu wa Congo) na Therese Kayikwamba Wagner ( Waziri wa Mambo ya Nje) imefanikiwa kumu outsmart Kagame na kumfanya awe uchi kwenye jumuiya ya Kimataifa hadi kufikia kuwekewa vikwazo na Mataifa ya Marekani, Canada, Uingereza, Ubelgiji na Ujerumani.
Mawaziri hawa kwa nyakati tofauti waliweza kutumia uzoefu wao kimataifa kuushawishi ulimwengu kuamini kuwa shida ya Congo Mashariki ni Kagame na sio siasa za ndani za Congo DRC.
Kwenye hili, Tanzania tuna la kujifunza sana hasa namna ya kuwatumia Diaspora ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa branded kuwa sio Wazalendo.
Kwenye hili tumejifunza kuwa Diaspora wanaweza kuwa Wazalendo kwa kulipigania Taifa kuliko watu waliopo ndani. Mfano Congo Jeshi linakimbia na kuwaachia Rwanda /M23 maeneo wakati hawa mawaziri Diaspora wanapambana Rwanda awekewe vikwazo na wanafanikiwa.
Tanzania tujifunze namna ya kuwatumia Diaspora kwa Congo DRC.
Picha:
Waziri Mkuu wa Congo DRC Bi Judith Suminwa Tuluka na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo DRC Therese Kayikwamba Wagner!