Matumizi ya pilipili katika tiba

The redemeer

JF-Expert Member
Jan 28, 2025
1,434
2,566
Pilipili ni ndugu zetu toka katika falme za mimea ( plant Kingdom).

Kama ninavyosema, na leo narudia, Kila kiumbe kina roho na mwili, hivyo hakina kazi moja tu, kila hicho kina kazi zaidi ya moja.

Pilipili ni kiungo na ladha katika chakula. mbali na vitamini nyingi ndani yake, Pia ni dawa katika miili ya watu.

Naweza kutaja virutubisho vyote vinavyopatikana katika pilipili lakini nitachelewa kutoa tiba. Hivyo ukitaka kujua pilipili ina virutubisho gani, kaulize Ikonda au Moi.

Pili pili ni moja ya kiungo muhimu sana India, ila ni kiungo hatari sana Tanzania.
Sababu inachangia vidonda vya tumbo.

Kama kawaida yangu usiponielewa basi nipo kinyume.
Pilipili ni tiba ya Magonjwa Mengi ila nitakupa mawili makubwa.
Akina dada, wanaopitiliza hedhi, Na wengine wenye vidonda sugu vya tumbo.

Dawa ya moto ni moto, basi na dawa ya vidonda vya tumbo ndiyo inasemekana inasababisha vidonda vya tumbo.

KUWA MAKINI.

Matabibu wanalijua hili, ila hawawezi kukwambia ili uwe mteja wa hospital na dawa zao zenye kemikali.

Pilipili nyingine kweli ni chanzo cha madonda tumbo, hivyo nielewe vizuri ni pilipili ipi sumu na ipi ni dawa.

Pilipili ambayo ni dawa ni pilipili kichaa kubwa. zile ambazo ni nene na ndefu. Maarufu kama pilipili za kihindi.

MADONDA TUMBO
Kwa wenye vidonda tumbo unaweza kutumia pilipili mbili, kwa kuzichanganya na mchuzi, uji, juisi, au chochote kitakacho kusaidia kuipunguza makali.

kisha utakunywa/ kula, mala mbili kwa siku. Yaani mchana na jioni. au muda wowote utakao kuwa na umbali sawa na mchana na jioni. Utatumia mpaka utakapohisi umepona.

Kitu cha kushangaza, Mungu alijua pilipili inawasha hivyo aliifanya itibu haraka, wengi hutumia siku mbili, tatu au wiki wanakuwa wamepona kabisa.

WANAOENDA HEDHI MFULULIZO

Kwa dada zangu wenye kupitiliza siku wakiingia katika hedhi, na hata wenye shida ya hedhi mfululizo.
Tumia pilipili, utapona achana na mambo ya kila kitu hospital.
Wazee wetu waliishi bila hospital muda mrefu na kufa wakiwa wazee wenye afya.
Pia kama una kidonda kinatoa damu, unaweza ukapaka hiyo pilipili. Damu itaacha kutoka.
 
Asante studio
 
Back
Top Bottom