Matukio ya nyuma yaliyopokelewa na kuungwa mkono kwa mihemuko na baadae kushindwa kuleta matokeo chanya na hatimae kutupwa

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,692
Ninaanze na:

SIASA ZA UJAMAA NA KUJITEGEMEA;

Kwa kifupi siasa hizi za ujamaa ndo nchi ilianza nazo,siasa zilisema njia kuu za uchumi ziwe mikononi mwa umma, biashara zilifanywe na serikali mfano usafirishaji KAUDO ,KAUMA, SHIRECU ,TACOSHIL na ATC etc, mashirika ya biashara mfano National milling , RTC, KABIMITA, UFI,MECCO etc, Siasa hizi zilianza baada ya uhuru mwaka 1961 ziliendelea wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hadi kushindwa na kufutwa rasmi mwaka 1992 wakati wa utawala wa awamu ya pili.

VIJIJI VYA UJAMAA

Iliitwa operationi vijiji, watu walihamishwa katika makazi yao na kupelekwa kwenye vijiji vya ujamaa na magari ya serikali, kule walipewa mablanketi na vitu vyao kulundikwa ardhini baadae operationi hii ilishindwa kuwa endelevu ikafa na watu wengi kurudi katika makazi yao ya awali. Hii pia ilitekelezwa na serikali ya awamu ya kwanza, ilishindwa vibaya sana.

AZIMIO LA ARUSHA

Azimio hili Mzee Oscar Kambona ( ni mmanda wa Mbinga Mbambabay) alilipinga kwa nguvu zote na aliamua kuhama nchi na Kuishi uhamishoni. Azimio la Arusha ilikuwa ni muendelezo wa siasa za ujamaa kwamba njia kuu za uchumi kuwa mikononi mwa umma na liliweka miiko ya viongozi, lilisema kiongozi asiwe:

Na mishahara miwili, na nyumba za kupangisha, na hisa katika makampuni ya kibepari, bepari au kabaila, mnyonyaji. Watu walilipokea kwa mihemko walitembea kwa miguu umbali mrefu mfano Mwanza hadi Dar-es-Salam kuunga mkono AZIMIO wengine walifia njiani mfano Seti Benjamin alifia njiaani kwa kugongwa na gari. Azimio lilipelekea umasikini wa kutisha kwa raia wa kawaida kwa sababu njia mbadala wa kujiongezea kipato zilipingwa na Azimio. Hatimae azimio lilifutwa na Azimio linguine la Zanzibar mwaka 1992 ambalo liliruhusu kufanya yote yaliyokatazwa na azimio la Arusha.

Azimio la Arusha makali yake yalianza kung`ata wakati waasisi wake bado wapo ( Mzee Nyerere na Kawawa).

KWA HIYO BASI;

Na sasa mkataba na DP WORLD Kwa vyovyote kama mkataba huu utakuwa na makali hapo baadae basi watu kama akina Wasira watakuwa hawapo kwa hiyo Mzee Wasira hana haki yoyote ya kumshambulia Tundu Lissu kwa maneno makali kwa sababu mkataba huu ukiwa na siki au sifongo au ukiwa shuburi hapo mbeleni yeye kwa umri wake atakuwa hayupo.

Pia Mzee Wasira akumbuke wakati tunaanza mfumo wa vyama vingi, yeye mwenyewe aliukataa mfumo huu akisema utaleta vita na katika kura za maoni kukataa au kuukubali mfumo huo watu asilimia 80 waliukataa na asilimia 20 kuukubali mwisho wachache ndo waliosikilizwa. kwa hiyo mkataba na DP WORLD unaweza kuwa na sinerio hiyohiyo hivyo basi Mzee Wasira anatakiwa kuweka akiba ya maneno. Pili CCM hawapashwi kumtumiam Mzee huyu kwa sababu aliwahi kuipinga CCM na kuwa mbunge kwa tiketi ya NCCRA wakiwa pamoja na TUNDU LISSU, iweje leo amwite tapeli wa kimataifa? Tundu Lissu akiwa ni tapeli wa kimataifa basi yeye WASIRA ni tapeli wa hadi sayari zingine.
 
Wasira ni janga la taifa
 
Back
Top Bottom