Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 26,226
- 19,121
Ndugu zangu Watanzania,
Nitawaleteeni Matukio Makubwa yaliyotikisa Nchi yetu na kuteka hisia za Watu wengi sana hapa Nchini. Nitakuwa nawaleteeni awamu kwa awamu.Leo naaanza na haya yafuatayo.
Tukio la Kwanza lilikuwa ni lile la kufariki kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Hayati Edward Ngoyai Lowassa .
Huyu waweza kusema ndiye Mwamba Mwenyewe wa kaskazini aliyestahili kuitwa hivyo na atakaye bakia katika kumbukumbu za mamilioni ya watanzania kama Mwamba kwelikweli na Jabali la Siasa za Nchi hii kutoka ukanda wa kaskazini
Ambaye alikuwa anakubalika na kuheshimika ukanda huo kupata kutokea kwa Miaka ya hivi karibuni au waweza kusema katika Historia ya Taifa letu. Alipendwa na watu wa vyama vyote na kuheshimika sana.alikuwa na mtandao mpana utafikiri mashirika ya ujasusi na upepelezi ya Marekani yaani CIA na FBI au MOSSAD ya Israel.Alikuwa na watu wake wa kumuunga mkono kila eneo na kila kona na kila taasisi au idara.
Alikuwa anakubalika kuliko Mwanachama Mwingine yeyote yule aliyekuwa anahitaji Urais kupitia CCM 2015.Na kama jina lake lingetua Mkutano Mkuu basi Moto Ungewaka kwelikweli.Ni huyu Mwamba na Jabali huyu alipelekea wajumbe kuimba mbele ya Mwenyekiti kuwa wana Imani na Huyu Mwamba.
Alikuwa na Nyota ya kipekee sana na upepo wa kukubalika kwa watu. .niliona watu wakideki barabarani ili apite utafikiri Rais Wa Marekani Barack Obama anatua Nchini.Alikuwa na Moyo wa kipekee sana.alikuwa mpole, mnyenyekevu,mwenye subira, uungwana,ukarimu na Upendo mkubwa sana kwa watu.
Alikubalika na watu wa Dini na madhehebu yote .hekima zake zilipita kiwango cha ubinadamu.utulivu wake ulikuwa wa kiwango cha juu sana.alitukanwa sana lakini hakumjibu mtu bali alisema anamuachia Mungu tu.
Huyu Mwamba alikuwa na Kambi nzito kwelikweli ya watu wazito kwelikweli nyuma yake.alikuwa ni kama taasisi ndani ya taasisi,chama ndani ya chama,mfumo ndani ya mfumo.Hata katibu Mkuu wetu wa sasa wa CCM Mheshimiwa Balozi DKT Emmanueli Nchimbi alikuwa upande wake, Mheshimiwa Hussein Bashe , Mheshimiwa Sofia Simba wote walikuwa upande wake.Kutangazwa kwa kifo chake mnamo February kulileta Simanzi na masikitiko makubwa sana.watu waliumia sana.waliomkosea wakati wa uhai wake walitamani afufuke wapate walau nafasi ya kuomba msamaha na kusamehewa.lakini haikuwezekana kwa sababu Mwamba na Jabali huyu alikuwa Amelala Usingizi wa Milele😭😭.
Tukio la pili lilikuwa ni lile la kifo cha Hayati All Hasssan Mwinyi la Mwezi Februari 29.Huyu ni Baba wa demokrasia,baba wa Uchumi na kwa hakika waweza kusema ni Baba aliyelitoa Taifa hili katika Umasikini mkubwa na kuanza kutengeneza matajiri wa kitanzania.ni huyu mzee wetu aliyewafanya Watanzania walau waache kuvaa suruali na nguo zenye viraka na kuanza kuvaa nguo nzuri. Ni huyu mzee wetu aliyefungua uchumi wetu na kuanza kukaribisha wawekezaji na uwekezaji na kukuza sekta binafsi.
Ni huyu mzee wetu aliyetoa uhuru wa kiuchumi kumilikiwa na watu binafsi pasipo hofu wala wasiwasi.kwa hakika kifo chake kiligusa sana hisia za watanzania na kuumizwa sana na kifo chake.hakuwa na baya na mtu mzee wa watu.hakuwa na makuu wala kiburi.kwa hakika huyu mzee anasehemu yake huko aliko.
Alikuza wanasiasa wengi sana na kuwaibua.Na kwa kukusaidieni ni kuwa huyu Mzee ndiye aliyempandisha na kumuweka katika Ramani ya kisiasa Rais wetu mstaafu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumteua na kumfanya kuwa Waziri wake.
Tukio lingine ni lile la mabadiliko ya a Baraza la Mawaziri lililofanywa na Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.ambapo katika mabadiliko hayo ilishuhudiwa Mheshimiwa January Yusuphu Makamba Mtoto wa Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM pamoja na Mheshimiwa Nape Moses Nauye Mtoto wa Mzee Moses Nauye rafiki Mkubwa pia wa Mzee Yusuphu Makamba wakiwekwa pembeni katika mabadiliko hayo ya Baraza la Mawaziri.
Mabadiliko haya yalimuibua hadi Mzee Yusuphu Makamba Mwenyewe aliyesema kuwa tusije kushangaa wakirejeshwa tena.
Tukio hilo liliibua na kuteka mijadala mingi sana ya kisiasa Nchini baada ya kuwekwa pembeni kwa vijana hao waliokulia ndani ya CCM na wenye Damu ya CCM na ambao wamepata bahati ya kuwa na wazazi wao wenye majina Makubwa ndani ya CCM.
Tukio la Mwisho kwa leo Ni lile la Tundu Antipas Mugwai Lissu ,Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kubadili Gia angani na kuamua kutangaza nia na hatimaye kuchukua,kujaza na kurejesha Fomu ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa.nafasi ambayo alikuwa amesema hawezi kuwania wala kushindana na kugusa Fomu itakayoguswa na Mwenyekiti wake.kitendo cha kubadili Gia angani na kutangaza nia kiliteka hisia za wengi,kukigawa chama,kuwagawa watanzania wanaofuatilia siasa za Upinzani na kuonyesha rangi ya kila kiongozi ndani ya CHADEMA.
Kwani tukio hilo lilishuhudia likiwagawa viongozi mbalimbali na wa mabaraza yake na kila mmoja akitupa maneno upande wa pili japo wote ni wa chama kimoja.tukio hilo la Lissu kutangaza nia limeshuhudia kupakana matope,kuchafuana ,kuleta sintofahamu,kuwagawa wanachama,wazee ,vijana,vyama mbalimbali kila mmoja akitoa mtizamo wake.
Uchaguzi huu wa CHADEMA hasa wa nafasi ya mwenyeketi wa chama Taifa linaendelea kuteka mijadala mbalimbali ya kisiasa hapa Nchini pasipo kuzimika wala kupoa siku hadi siku .na inatarajiwa kuanzia Januari mosi moto utawaka zaidi na makombora kurushwa zaidi na zaidi na kila aina ya silaha za maneno,shutuma kurushwa kwa nguvu sana.
Hili tukio halitapoa kwa sasa bali litakuwa ni la kufungia na kuanzia mwaka Mpya.
Kwa leo Mimi Mwashambwa Lucas Mchambuzi wa masuala mbalimbali na kada kindakindaki na Mtiifu wa CCM naishia hapa na nitaendelea wakati mwingine wowote ule nikipata nafasi.usikose kunifuatilia maandiko yangu ili usije kujutia na kubakia ukibubujikwa na machozi ya huzuni.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.