KERO Matokeo ya wanafunzi wa Stashahada 2014/2017 NACTVET toka 2017 hadi sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni muhitimu wa Stashahada ya maabara ya binadamu (Diploma in Medical Laboratory Technology) 2014/2017 katika chuo cha St. John’s university of Tanzania Dodoma.

Toka nimemaliza 2017 matokeo yetu hayajapelekwa NACTIVET hivyo kuleta ugumu pale tunapotakiwa kuomba vyuo kwaajili ya kujiendeleza kwa elimu ya juu kwasababu ya kukosa award verification number (AVN).

Tumejaribu kufuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio tunaomba mtusaidie kupaza sauti.
 
Back
Top Bottom