LGE2024 Matokeo ya uchaguzi mtaa wa Geza Ulole, Kigoma yabatilishwa na Mahakama

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

upupu255

Member
Sep 4, 2024
85
132
Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imebatilisha matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Geza Ulole, Manispaa ya Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma, na kuamuru uchaguzi huo urudiwe baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu na miongozo ya uchaguzi.

Uamuzi huo umetokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa mtaa huo kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, ambaye hakuridhika na matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi.

Akizungumza na Jambo TV baada ya hukumu hiyo, Wakili Thomas Msasa amreleza kuwa moja ya sababu za kufungua kesi hiyo ilikuwa ni uwepo wa kura feki ambazo zilidumbukizwa kwenye masanduku ya kura na baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi, kitendo ambacho kilishuhudiwa na mawakala wa uchaguzi na kuthibitishwa mahakamani.

"Tuliweza kuleta mashahidi waliothibitisha kuwa baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi walidumbukiza kura feki kwenye sanduku la kura, na mawakala waliwakamata wakifanya hivyo. Mahakama imethibitisha kuwa uchaguzi wa Geza Ulole haukufuata taratibu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa," amesema Wakili Msasa.

Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa, mahakama ilibaini kuwa vitendo hivyo, pamoja na ukiukwaji mwingine wa taratibu za uchaguzi, vilihalalisha kufutwa kwa matokeo na kuamuru uchaguzi huo urudiwe.

Soma, Pia: Kigoma: ACT Wazalendo kufungua kesi kuwashtaki Wasimamizi wa Uchaguzi
 
Wakati act wakipinga matokeo mahakamani na kushinda wao wanapiga porojo hewa
 
Hata ukirudiwa wasimamizi ni wale wale DED/WEO/VEO hakuna la maana
Hiyo ndio changamoto.
Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imebatilisha matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Mtaa wa Geza Ulole, Manispaa ya Kigoma Ujiji, mkoani Kigoma, na kuamuru uchaguzi huo urudiwe baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu na miongozo ya uchaguzi.

Uamuzi huo umetokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa mtaa huo kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, ambaye hakuridhika na matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi.

Akizungumza na Jambo TV baada ya hukumu hiyo, Wakili Thomas Msasa amreleza kuwa moja ya sababu za kufungua kesi hiyo ilikuwa ni uwepo wa kura feki ambazo zilidumbukizwa kwenye masanduku ya kura na baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi, kitendo ambacho kilishuhudiwa na mawakala wa uchaguzi na kuthibitishwa mahakamani.

"Tuliweza kuleta mashahidi waliothibitisha kuwa baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi walidumbukiza kura feki kwenye sanduku la kura, na mawakala waliwakamata wakifanya hivyo. Mahakama imethibitisha kuwa uchaguzi wa Geza Ulole haukufuata taratibu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa," amesema Wakili Msasa.

Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa, mahakama ilibaini kuwa vitendo hivyo, pamoja na ukiukwaji mwingine wa taratibu za uchaguzi, vilihalalisha kufutwa kwa matokeo na kuamuru uchaguzi huo urudiwe.

Soma, Pia: Kigoma: ACT Wazalendo kufungua kesi kuwashtaki Wasimamizi wa Uchaguzi
Ni aibu sana kwa chama cha mapinduzi CCM, kwani hamjiamini !?
 
Back
Top Bottom