Matatizo ya nchi hii mengi yanatokana na kutoheshimu ujuzi na nidhamu

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
9,133
5,028
MATATIZO YA NCHI HII MENGI YANATOKANA KUTOKUHESHIMU AKILI KUBWA.

Na Thadei Ole Mushi.

Morogoro wametangaza Mgao wa Maji, Dar wameshatoa ratiba ya mgao wa maji, Huko mjini kila mahali Majenereta yananguruma kuashiria kuwa kuna tatizo la Umeme japokuwa waziri January hajatutangazia.

Tuliwapa Malaysia Mbegu ya Mchikichi toka Kigoma leo ni nchi ya pili Duniani kwa uuzaji wa Madufuta ya Michikichi. Na dili hili la Michikichi linachangia pato la Malaysia asilimia 2.7 ya GDP ya taifa hilo.

Singapore ilipata Uhuru kabla yetu ila wapo mbali mno.... Hatufanani nao hata kidogo lakini ukiwauliza Siri kubwa ni nn wanakuambia walikubali kubadilisha mfumo wa kuchaguana. China nao vivyo hivyo siri kubwa ni mfumo wa kuchaguana....

π‘»π’–π’‹π’Šπ’Œπ’–π’Žπ’ƒπ’–π’”π’‰π’† π’Žπ’Šπ’‡π’–π’Žπ’ π’šπ’‚π’ π’Šπ’‘π’π’‹π’† π’šπ’‚ π’Œπ’–π’‘π’‚π’•π’‚ π’—π’Šπ’π’π’ˆπ’π’›π’Š.

πš‚π™Έπ™½π™Άπ™°π™Ώπ™Ύπšπ™΄

Kishore Mahbuban ambaye aliwahi kuwa President of the United Nations Security Council kati ya mwaka 2001 and 2002 anasema....

Siri kubwa ya Singapore kuondoka kwenye umaskini walifanya mambo matatu waliyoyapa formula ya MPH. M kwa maana ya Meritocracy namna ya kupata best people na kuwapa uongozi. Anadai waliachana na issue ya kuwapa mjomba, Shangazi, binamu madaraka na badala yake wakatafuta the best people kwenye nchi yao. Anatolea mfano wa Lee Hsien Loong na Lee Kuan Yew kama wanafunzi bora kabisa wa Singapore waliosoma Havard namna walivyowatumia kubadili Singapore yao. Fuata link ifuatayo kumsikiliza;-


𝙲𝙷𝙸𝙽𝙰

Zang Weiwei huyu ni profesa toka pale chuo kikuu cha Hudah tumiwahi kufafanua hapa namna na wao wanatafuta viongozi pale China kuwa hutoki from no where kuwa kiongozi bali wanakutayarisha na kukufuatilia toka ngazi za chini. Pitia link pia kumsikiliza ....


Hakuna haja ya kibishana kama tunahitaji kusogea hakuna miujiza. Use your best people kwenye maamuzi ya nchi hii.

Mimi naamini Umri wa Miaka 60 ya Uhuru ingetosha kumalizana kabisa na huduma za msingi za Wananchi. Wenzetu wanafikiria mambo ya Artificial intelligence sisi bado hatujamaliza kugawiana umeme na maji. Haya mawili ya Umeme na Maji yanatokea nchi ikiwa na rasilimali lukuki...

TANZANIA

Ni ya kwanza duniania kwa uzalishaji wa madini ya Tanzanite.

Ni nchi ya nne kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu duniani.

Ni nchi ya kwanza Afrika kuzungukwa na maji kila pande ukiachilia nchi zinzoundwa na visiwa.

Ni nchi yenye ititiri wa mito na maziwa yenye maji yasiyo na chumvi kabisa. Tanzania ina mito zaidi kumi yenye maji muda wote wa mwaka na ni ya nchi pekee Afrika ambayo kati ya maziwa 10 makubwa duniani Tanzania pekee inaingiza maziwa matatu (Victoria,Tanganyika na nyasa)

Ni nchi inayohudumia nchi sita zisizokuwa na Bandari kama vile Uganda, zambia, Congo, Rwanda, Malawi na Burundi.

Tanzania ina Bahari kubwa tu ya Hindi watu wanavua na Kuoga huko.

Tanzania ina ardhi yenye Rutuba ya Kutosha ambayo inastawisha tu vichaka huko maporini.

Tanzania haijawahi kupigana vita toka imepigana ile ya Uganda, wala haijawahi kukumbwa na majanga makubwa ya magonjwa na mafuriko au tetemeko la Ardhi ikilingsnishwa na nchi nyingine Duniani na Afrika.

Tanzania imefanikiwa kudumisha amani yake kwa muda mrefu sana. Hivyo inatoa fursa kwa watu kufanya kazi.

Tanzania ina Gesi asilia isiyomithilika Duniani kwa Afrika ni ya kwanza....

Tanzania ni ya Kwanza kuwa na Mbuga za wanyama Afrika na ya pili kwa vivutio vya utalii Duniani inaifuata Brazil.

Tanzania ina Madini mengi mno ukiachilia Dhahabu na Tanzanite ambazo nimeshazitaja. Ina kiwango kikubwa cha Almas, Nikel, Rubi, Uranium, magadi Soda,Graphate,Tancoal, makaa ya mawe, chama na mengineyo mengi. Na kila madini hapo unakuta kama si ya Kwanza ni ya Pili.

HUWA NARUDIA NA NITAENDELEA KURUDIA.

Mfumo wa Upatikanaji wa Viongozi kwenye taifa hili una mapungufu mengi sana. Ukitaka kuamini angalia tu kwenye jimbo lako watia nia wanaotaka kuwania ubunge 2025. Je wanaotaka kugombea wana majibu ya matatizo yetu kama Taifa?.

Mkipata Muda pitieni Mawaziri wanaounda baraza la mawaziri la Kenya. Wote wanasifa zinazofanana fanana wametokea kwenye misingi ya kibiashara. Wamechaguliwa very Strategic kwa ajili ya wote ku commercialize sector zao.... Dunia inakimbia sana lazima tukubali kukimbia au hata kudandia mitumbwi ya wengine.

Katiba yao inaruhusu kutoka nje ya wabunge na kwenda kuchagua watu wa kuja kuwa mawaziri. Kwao hata kama wabunge wakiwa wabovu kiasi gani haiwezi kuathiri Serikali moja kwa moja kwa kuwa watendaji wakuu wanafanyiwa vetting nje ya mfumo wa kuchaguana.... hapa unaweza kuamua kuingiza akili zako zote kubwa kukuzunguka.

Kwa Tanzania hawa wanaoonyesha nia ya kugombea ubunge 2025 asilimi 80 ndio watakuja kuwa Mwaziri. Tumempa Rais Nafasi Kumi tu za kuangalia kama huko nje kuna watu makini wa kuwachagua kuingia ndani na kuja kumsaidia. Japokuwa bado wanaorudishwa kuja kusaidia ni wale wale huenda kwa kulipa fadhila au kwa kuwa ni ndugu wa viongozi flani flani Serikalini.

CCM ifanye nini?

Kwanza tukumbuke haitaki kuachia madaraka, la pili tukumbuke wanaoonyesha nia ya kugombea sasa ndio mawaziri wetu wa Kesho. Kama kweli tunataka Rais aje azungukwe na vichwa vya taifa hili lazima tukubali kuanzisha mradi wa kuwaandaa wabunge wa 2025. Sina Ugomvi na Mawaziri au wabunge waliopo huenda wanaweza sana ila bado hawajatuonyesha kama kweli wanaweza kwa kuwa pamoja na rasilimali tulizonazo matatizo yetu ni yale yale.

Tunahitaji sana kufikiria Solutions za matatizo yetu katika angle nyingine, Mfano tuchukulie mabwawa yanayozalisha umeme na Mito inayotoa maji ikikauka tutakufa kwa kukosa maji na Umeme? kuna nchi ambazo ni jangwa kabisa lakini hizo hekaya za abunuwas hawana kabisa.

Kila kitu Mungu katupa tukubali kubadilika tusogee au tuamua kukaa hapa hapa na umasikini wetu.

Comment then Share....

Ole Mushi
0712702602
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…