Matatizo tuliyoyaficha kwa siku mbili kwa kujidanganya hayapo, yamerudii upya

the guardian 17

JF-Expert Member
Aug 15, 2024
353
515
Kutokana na mkutano wa nishati wa viongozi wa Afrika barabara zikafungwa, kazi zikasitishwa, wanafunzi wakasalia majumbani. Tukayaficha matatizo ya jiji la Dar es salaam kwa muda. Ingawa nayo ilituchoresha kwa kuonesha namna gani hatuna miundombinu ya kutosha hadi kusitisha baadhi ya huduma.

Leo changamoto zimerudi palepale, foleni ndefu, adha ya usafiri kwa wanafunzi, msongamano kwenye vyombo vya usafairi wa umma.

Nadhani sasa ni wakati wa kuboresha miundombinu tuliyonayo kwa kiwango kikubwa kuendana na kasi ya ukuaji wa Jiji hili la hekaheka, na kibiashara ili tuachane na hizi mambo za kuficha matatizo kwa muda ukija ugeni mkubwa kwa kujidanganya kuwa hayapo.
 
Back
Top Bottom