Mambo mengine ni ya kujitakia, wala hakuna cha dawa wala nini. Kama ni dawa sijui uchawi tuambie unafanyaje kazi mpaka kweli ufanyiwe hivyo. Wale wezi wanatumia psychology kutokana na muonekano wa mtu, na jinsi anavyotembea, na kushangaa shangaa kila kitu anachokiona, na kutazama vitu vya kawaida kwa muda mrefu.
Askofu Dr Gwajima alishatoa ushauri wa kupiga selfie kwanza na kutuma instagram kabla ya kuendelea na shughuli nyingine.
Ushauri wangu, watu mnapokuwa na fedha nyingi na kuwepo barabarani mjitaidi kuwa wawili, halafu hakuna kuongea na mtu wala kupoteza muda wa kusimama simama.