Matangazo ya makampuni ni anasa katika nchi yetu masikini!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,532
Nimejaribu kuangalia uwekezaji wa baadhi ya makampuni hasa haya makampuni ya simu nikaona kuwa yanatumia gharama kubwa sana.

Hii inanifanya nifikirie kuwa kuna umuhimu wa kuwa na regulatory body ya kufuatilia gharama hizi zinazotumiwa na makampuni kufanya matangazo ambayo hayana thamani na fedha inayorumika...

Ushauri wangu ni kuwa hizi fedha zinazotumika kwenye matangazo ni vyema zikaelekezwa kwenye ununuzi wa madawati ambapo tumeshuhudia kuna upungufu mkubwa.

Isitoshe makampuni haya yanawezekana kuwa yanatumia fedha nyingi sana katika matangazo badala ya kulipa kodi stahiki.

Hebu wabunge watunge sheria ya kudhibiti matumizi yasiyo na tija kwa makampuni haya ambayo yanalipa kodi kiduchu kulinganisha na wanachokipata.
 
Mkuu matangazo ni mfumo wa masoko katika kutangaza bidhaa au huduma, hivyo ni lazima matangazo yawepo kwa kila kampuni.

Na katika biashara ya ushindani kama ya mawasiliano, matangazo hayakwepeki.
Tusifute matangazo bali turegulate fedha inayotumika ilihali nchi hii ni yamasikini.

Inashangaza kuona tangazo la kampuni likiwa la bei ghali sana huku wizara ya afya ikipewa msaada wa matangazo na wamarekani.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Eti wakanunue madawati
Khaaa kwani serikali inafanya kazi gani?
Kodi wawalipe afu madawati wawatengenezeee
Kodi wanayolipa ni ndogo sana kulinganisha na wanachokipata
 
Duniani kote marketing costs ni pasua kichwa kwahiyo kama unadhani ni namna ya ukwepaji kodi basi duniani kote kampuni za kibiashara zinakwepa kodi kupitia marketing and advertisement... in short, ni inevitable and you can't tell any business firm to stop marketing!

Mleta mada, nadhani hili eneo la biashara si lako!
 

"". It's either u market ur products or quit business !! " !

Matangazo yanalipiwa ndo maana tuna tv , billboards , magazetini, radio ! Bila matangazo hivi vyote ni nothing ... Kwa hiyo tambua kwamba advertising and marketing in general is a cross cutting function
 
Sijaongelea kuhusu kusitisha matangazo ya biashara ...naongelea gharama zake zinazotaka kufanana na nchi zilizoendelea ..
My observation ni kwamba makampuni haya yanavuna fedha za masikini na fedha hizi hazitumiki kuwakomboa masikini hawa!
 
Kwa Hali inavokwenda utatupangia mpaka sokoni tukatumie sh.ngapi, ama mtu matumizi ya siku asizidishe 30,000.
 
Tusifute matangazo bali turegulate fedha inayotumika ilihali nchi hii ni yamasikini.

Inashangaza kuona tangazo la kampuni likiwa la bei ghali sana huku wizara ya afya ikipewa msaada wa matangazo na wamarekani.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Lakini hizi fedha za matangazo si ni za kampuni husika?

Hizi fedha hazihusiani kabisa na fedha za walipa kodi.
 
Rejea mada yangu viziri...wewe unaona ni sawa kutumia milioni kumi kwenye matangazo wakati kuna watoto wanakaa chini?halafu matangazo yenyewe yanamlenga mtu anayelala njaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…