Wasalaam Wana jamvi, nimejaribu kufanya utafiti wangu kwenye maagizo, ama matamko mengi yanayo tolewa na viongozi wetu kwa Sasa yamezaa matunda ktk idara nyingi na taasisi nyingi. Kwa mfano, lile agizo la kuzuia viroba, muda wa mwisho kwa bodaboda, kuto kunywa Pombe mchana, abiria wa bodaboda kuvaa kofia nguumu. Na mengine mengi. Nia ya viongozi na dhamira ya maagizo hayo, natumaini ilikuwa ni nzuri. Lakini ni tofauti na vile utekelezaji wake ungetakiwa. Matokea yake imekuwa ni mianya ya rushwa kwa watekelezaji. Naona tuwe tunaangalia na namna ya kuwaelimisha watekelezaji wa maagizo haya wawe wanafanya kwa uadilifu. N. B na hili lipo ktk sehemu nyingi, ikiwapo zoezi la kuondoa machangudoa, sakata la madawa ya kulevya n.k. naomba kuwasilisha.