Matajiri wakubwa Tanzania hawana msaada wowote kwa jamii zaidi ya kuinyonya

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
3,691
10,592
Nimekaa nakatafakari sana juu ya social benefits tunazopata kama jamii kutoka kwa Hawa tunaowaita businesses bundit wa hapa nyumbani.

Kuanzia kwa Mohamed Dewj, Salim Bakhresa, Assas na wengine wengi hawana msaada wa moja kwa moja kwa jamii zaidi. Hivi kweli hizo Foundation wanazoanzisha mfamo Mo foundation imesaidia vijana wangapi kimasomo kama siyo uhuni tu.

Hawawazi kurudisha kwenye jamii kile wanachochukua japo kwa uchache kupitia huduma za afya ama elimu. Mabilioni wanayoyachukua kupitia biashara jamii haipati chochote zaidi ya ajira za ujira mdogo kwa vijana kwenye viwanda vyao.

Hawa matajiri wanatakiwa wasaport elimu kwa kutoa ufadhiri wa masomo angalau kwa vijana wachache, watoe pesa kwa ajili ya matibabu kwa wazee ama lishe kwa watoto na siyo kuchukua tu na kujimilikisha. Wenzako nchi nyingine wanatoa saport kubwa kwenye mambo ya kijamii.

Tunataka kuona mchango wa moja kwa moja wa wafanyabiashara wakubwa kwenye afya, elimu na huduma zingine na siyo kuhusika kwenye michezo na sekta ya entertainment pekee.
 
Hakuna aliyekatazwa kuwa tajiri na nadhani cha kuwauliza ni kama wanalipa kodi stahiki. Kama wanalipa then kinachobaki ni jukumu la hao wanaonunua V8 mpya Ila vyoo vya madarasa tunasubiri ufadhili wa marekani
 
Umesema kweli...
Nlishuhudia watoto wa Bakharesa wakiendesha Gari za kifahari hapa Bongo.

Kuna haja ya kuwakumbusha waige Mfano watajiri Mengi
Duniani hakuna cha bure. Wao wamepigana kupata utajiri nyie mnadai wawagawie? Mliwasaidia kutafuta? Nchi ina raslimali kibao, hangaikeni na serikali iwe viongozi wanaowajibika kwa wananchi.
 
Umesema kweli...
Nlishuhudia watoto wa Bakharesa wakiendesha Gari za kifahari hapa Bongo.

Kuna haja ya kuwakumbusha waige Mfano watajiri Mengi
 
Nimekaa nakatafakari sana juu ya social benefits tunazopata kama jamii kutoka kwa Hawa tunaowaita businesses bundit wa hapa nyumbani.

Kuanzia kwa Mohamed Dewj, Salim Bakhresa, Assas na wengine wengi hawana msaada wa moja kwa moja kwa jamii zaidi. Hivi kweli hizo Foundation wanazoanzisha mfamo Mo foundation imesaidia vijana wangapi kimasomo kama siyo uhuni tu.

Hawawazi kurudisha kwenye jamii kile wanachochukua japo kwa uchache kupitia huduma za afya ama elimu. Mabilioni wanayoyachukua kupitia biashara jamii haipati chochote zaidi ya ajira za ujira mdogo kwa vijana kwenye viwanda vyao.

Hawa matajiri wanatakiwa wasaport elimu kwa kutoa ufadhiri wa masomo angalau kwa vijana wachache, watoe pesa kwa ajili ya matibabu kwa wazee ama lishe kwa watoto na siyo kuchukua tu na kujimilikisha. Wenzako nchi nyingine wanatoa saport kubwa kwenye mambo ya kijamii.
Duniani kote matajiri wanatunyonyq masikini

Ndio mfumo wa kibepari unavyofanya kazi
 
Kila kitu kinawezekana; tajiri namba 1-20, wakitumiwa vizuri wanaweza wakaleta maendeleo chanya kwa jamii na uchumi kuimarika.

Mfano:- tajiri namba 1, apewe mkoa wa Dar, Pwani, Tanga, Morogoro; aakikishe mikoa hiyo ina viwanda, mashamba makubwa ya kilimo, uvuvi wa kisasa, ufugaji wa kisasa; hivyo hivyo kwa tajiri namba 2, 3 n.k

Muhimu wapewe mazingira mazuri ya utendaji; na hakika ndani ya muda mfupi maendeleo yatakuwa makubwa sana.​
 
Back
Top Bottom