Daudi Kempu
Member
- Dec 6, 2024
- 22
- 51
1. Ni shughuli zipi zinakufanya ujisikie hai zaidi?
Yaani ni jambo gani ukilifanya unaishi ndani ya kulifanya, hata kama halikupi hatua kubwa kulifanya tu kunakupa amani ya ndani?
2.Ndoto zako za utotoni zilikuwa zipi? Binafsi utotoni nilikuwa na ndoto ya kuwa mwanajeshi, ila kila nilipojaribu kuiongelea nilikatishwa tamaa kwa kuambiwa mimi ni mfupi na jeshini hawapokei watu wafupi. Wewe utotoni uliota kuwa nani?
3. Ni nini ungefanya kama ungekuwa na uhakika kuwa huwezi kushindwa?
Swali hili nilijiuliza miaka mitatu iliyopita, na majibu niliyoyapata yamenisogeza hapa nilipo hivi sasa. Napenda kuandika, napenda kuelimisha, na isivyo bahati; hofu ya kushindwa ndo kitu kinachozuia wengi wetu kufanya vitu vikubwa. Fanya hicho unachotamani kufanya ukiwa ndani ya matarajio kidogo na jitihada kubwa, kuna siku utajishukuru kwa hilo.
4. Ungependa kukumbukwa vipi?
Kama ulizaliwa, ukala chakula cha wazazi, ukasomeshwa ukakosa ajira, ukadanga au ukabemendwa na mishangazi kisha ukafa, ndo itakuwa hadithi ya kweli ya maisha yako baada ya kuondoka katika ulimwengu huu, jitafakari upya. Mwenye kalamu ya kuandika namna anataka kukumbukwa ni wewe, na wakati ni sasa.
5. Ni ujuzi gani unaufurahia kutumia? Kwenye dunia tunajifunza mambo mengi haswa sisi tulioamua kuishi kama tuko darasani. Katika hayo uliyojifunza na ukayajua, ni jambo gani ama ujuzi gani unapenda kuutumia?
6. Ni masuala gani unayajali sana?
Je ni masuala ya wanawake na vijana kama mimi? Je ni maswala ya wababa? Je ni masuala ya utalii ama ukatili ama maendeleo ya jamii? Unajali mambo gani zaidi?
7. Ni nani anayekuhimiza/anayekupa hamasa na kwa nini? Ni nani 'roll model' wako? Ni nani unamtazama sana na unatamani ungekuwa kama yeye? Kwa nini? Hakikisha sababu isiwe "napenda tu alivyo na hela" utachekesha na utajikuta kwenye mtego wa uhalifu.
8.Siku yako kamili inaonekana namna gani?
Ni nini kikitokea kwenye siku yako unahisi imekamilika? Binafsi nikimpa mtu mmoja tabasamu na mimi nikatabasamu siku yangu inakamilika mapema sana.
9.Unajiona wapi baada ya miaka mitano? Kwanza nikwambie ukweli, huwezi kujiona popote kama hufanyi chochote cha maendeleo. Kama unalala na kuamka na kula ugali wa shkamoo halafu unajiona kuwa chief Goodlove, unatatizo la afya ya akili. Pale unapojiona kwenye ndoto zako, panahitaji mchakato wa 'do or die' ili kupafikia.
10. Ni hatua gani unaweza kuchukua leo ili kuzikimbilia ndoto zako?
Hili ni swali muhimu mno ambalo majibu yake unayo wewe; majibu yake yanapaswa kuendana ama kulandana sana na ndoto ulizonazo.
Kujifunza hakuna mwisho. Inuka, jipambanie, umasikini haujawahi kumfaa mtu kwa Namna yeyote ile"