Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 2,759
- 9,294
Kuanzia Ijumaa ya wiki iliyopita masoko ya hisa ya Marekani yameporomoka kwa kasi sana. Wachumi wanasema hii inaweza kupelekea kushuka kwa uchumi (economic recession) nchini Marekani na huenda sehemu nyingine duniani.
Siku ya Jumatatu 5 August 2024 peke yake kwa ujumla masoko makubwa ya hisa ya Marekani kama Nasdaq, S&P 500, Dow Jones yamepoteza $1.93 trillion.
Kuporomoka kwa soko la hisa Marekani kumeathiri makampuni saba makubwa ya teknolojia ya Marekani.
Ndani ya masaa 24 tu hisa za makapuni hayo zimeshuka sana

- Alphabet/Google: -11%
- NVIDIA: -11%
- Apple: -10%
- Meta: -10%
- Tesla: -10%
- Amazon: -10%
- Microsoft: -9%
Huenda mwingine asielewe hizo asilimia zina thamani gani. Hizi ni thamani ya pesa walizopoteza kwenye market cap:
- Nvidia : – $300 billion
- Apple : – $224 billion
- Amazon : – $109 billion
- Meta : – $102 billion
- Tesla : – $ 101 billion
- Microsoft : – $ 99 billion
- Google : – $ 98 billion
Kufuatia kuanguka kwa hisa imepelekea watu kupoteza pesa walizowekeza kwenye biashara ya hisa. Asilimia 55 hivi ya Wamarekani wamewekeza kwenye biashara ya hisa.
Baadhi ya mabilionea wa Marekani net worth za utajiri wao zimeshuka ndani ya saa 24 tu, hiki ni kiwango cha billions walizopoteza:
Baadhi ya mabilionea wa Marekani net worth za utajiri wao zimeshuka ndani ya saa 24 tu, hiki ni kiwango cha billions walizopoteza:
- Jeff Bezos (Amazon)– $8 billion
- Jensen Huang (Nvidia CEO) – $7.9 billion
- Mark Zuckerberg (Meta CEO) – $6 billion
- Larry Ellison (Oracle chairman) – $6 billion
- Elon Musk (Tesla CEO) – $6 billion
Kampuni ya intel yapanga kupunguza wafanyakazi 15,000.
- Kati ya kampuni zote, intel inapitia kipindi kigumu zaidi. Imepanga kupunguza wafanyakazi 15,000 ambayo ni sawa na 15% ya wafanyakazi wake, hii ni kufuatia kushuka kwa mapato na kudorora kwa hisa zake kwa 57% na kupoteza $30bn kwenye biashara.
"Mapato yetu hayajakua kama ilavyotarajiwa na bado hatujafaidika kikamilifu na AI."
Pat Gelsinger (Intel CEO)
Pat Gelsinger (Intel CEO)
Warren Buffet
Bilionea Warren Buffet anasifika sana kwa kuwa bilionea ambaye amefanikiwa hasa kuwekeza kwenye biashara ya hisa katika makampuni makubwa mbalimbali duniani kupitia kampuni yake inayoitwa Berkshire Hathaway.
Siku moja alihojiwa aliulizwa ni nini siri ya mafanikio yake katika hisa, uwekezaji ambao hupanda na kushuka leo unaweza kuamka tajiri kesho ukajikuta umeamka masikini?
"In order to make profit, you've to sell high. And to make more profits, you've to buy low."
Warren Buffett
Warren Buffett
Hiki ndicho alichokifanya Warren Buffet kabla ya mdororo huu wa masoko ya hisa. Huyu mzee amekuwa mzoefu kiasi cha kwamba ni kama anajua nini kitatokea.
Tuzungumzie eneo moja tu: Inafahamika kuwa legend Warren Buffet ana hisa Apple moja ya kampuni kubwa sana duniani katika market value.
Aliishangaza dunia June mwaka huu alipouza 55.8% ya hisa zake za Apple akabaki na cash. Wakati huo anauza ikumbukwe hisa za Apple zilikuwa na thamani kubwa.
Kipindi hiki cha mdororo katika masoko ya hisa, makampuni huwa yanashusha sana bei za hisa zao ili kuwavuta wawekezaji. Usishangae mzee Buffet akanunua tena hisa za Apple katika discount price au akanunua kwingine akiwa amejitengenezea faida maradufu au akaamua kuwekeza kwenye sekta nyingine kabisa nje ya biashara ya hisa. Hapa ndipo utamuelewa aliposema "In order to make profit, you've to sell high. And to make more profits, you've to buy low."
Watu 500 tajiri zaidi ulimwenguni wamepoteza jumla ya $134 billion ndani ya siku moja kufuatia anguko la masoko ya hisa Marekani.