Masikini kaya yetu...

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,582
Maskini kaya yetu.

Mababu zetu walikuwa huru kabla ya ujio wa wageni (Wazungu). Waliishi kwa amani na kwa kufuata utaratibu wa kimila uliokuwepo. Baada ya ujio wa wageni hao, waliwatesa mababu zetu na kuwafanya watumwa ndani ya ardhi yao.

Kundi dogo ndani ya kaya yetu walifanikiwa kuwaondoa hao wageni, kaya ikawa huru tena. Lakini maskini ndani ya kundi hilo dogo kulikuwepo wanakaya ambao walikuwa na chembechembe za unyanyasaji walizozicopy toka kwa wazungu.

Kundi dogo hilo machoni lilionekana kama linataka tuwe huru kumbe sio hivyo. Waliopingana na kundi hilo walifungwa kama sio kupandishwa vyeo na kuwa marehemu. Waliofungwa walibakia kukaa vyumba vya uhani.

Miaka nenda nenda rudi wakajitokeza wataka uhuru wa kweli lakini nao wamebakia kubezwa tu, na hii inatokana na kwamba wengi wa wanakaya yetu hawakupata elimu, hawawezi kung’amu jema na baya. Wao wakila na kulala wanaona kila kitu sawa tu.

Kwa sasa Kaya yetu imekuwa kubwa sana, kitu kinachofanya hata majirani zetu kujifanya wanakaya na kupata hata nafasi za kuwa viongozi wa kaya ili mradi tu wameunga mkono mawazo ya waliowafukuza wageni wa mwanzo.

Imefika hatua mbaya hata vikao vya kaya wanakaa wao peke yao ili wapitishe maamuzi ya kuendelea kutunyanyasa. Wametuzuia hata kutembelea majirani eti ukitaka kutembea mpaka uombe ruhusa toka kwa mkuu wa kaya, na mkuu wetu wa kaya hana hobby ya kutembea kabisa. Neno tembea uone kwake ni msamihati mkubwa sana.

Maneno ya mkuu wa kaya yanakuwa tofauti na matendo yake. Aliahidi kushirikisha wanakaya wote lakini imekuwa kinyume. Amezuia hata vikao vya familia zisizounga mkono itikadi zake. Ana kila dalili ya kulipiza kisasi kwa yeyote alomtenda ndivyo sivyo kabla ya kuwa mkuu wa kaya. Maamuzi yak wake hamshirikishi mtu, na ukithubutu kumshauri au kumkosoa ujue chumba cha uani ni halali yako.

Ee Mungu inusuru Kaya yetu, muinue Daniel ndani ya kaya hata akitumbukizwa ndani ya shimo la sImba aendelee kuiombea kaya yetu ili iwe huru kwani siku hizi hata mkate wa kila siku umekuwa tatizo. Watoto wetu wanasoma kwa shida, wagonjwa wananyimwa chakula ... mambo yamekuwa mambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…