mashplayer
Member
- Oct 25, 2011
- 14
- 22
Habari za Asubui wana JF,
Naomba kuleta mada kwenu kuhusu haya mashirika ya kigeni yanayojiita ya kusaidia binadamu (humanitarian) au kujiita mashirika ya kimataifa yasiokuwa ya kiserikali (INGO). kwa mfano; Medecins sans frontieres, Medecins du monde na mengine mengi.
Kwanza kabisa mimi ni mwajiriwa wa moja ya haya mashirika na kilichonileta huku ilikuwa sio mshahara au maslahi mazuri bali ukosefu wa ajira wa muda mrefu na kukaa sana mtaani bila kazi maalum.
Nilipata shavu kwenye hizi shirika za kigeni humanitarian, lakini nilichokutana nacho huku nafikiri sijawahi kutana nacho toka nimeanza kufanya kazi kwenye mashirika binafsi.
Kwanza kabisa ogopa shirika lenye chimbuko au kutokea uswisi au ufaransa, hawa jamaa ni wabaguzi sijawai kuona. Pili, viwango vyao vya mishahara ni vibovu sana na hata mazingira ya kazi kwa wazawa ni magumu sana. Kuna muda unajikuta upo kama mtumwa ndani ya nchi yako kwa sababu tu hauwezi kuacha kazi mana mtaani ni pagumu sana na kazi hakuna. na haya mashirika wanatumia kigezo hiko kama fimbo ya kuchapia wazawa.
Pia, wanatumia sana loop holes za sheria zetu za tanzania ili kutukandamiza, kwa mfano, kuna kitu kinaitwa internal regulations, hzi ni sheria za kikandamizi ambazo zimetungwa kulingana na sheria ya ajira ya Tanzania lakini wametumia mianya ya sheria hiyo ili kuwabana national staff.
Tukirudi kwenye mishahara, mtu anaitwa officer mshahara unaanzia laki 8 take home na hata kama ulitoka sehemu unalipwa zaidi watakuambia wao salary grid yao ipo fixed na hakuna makubaliano yoyote au negotiations zozote.
Hata ufanye kazi kama punda siku saba za wiki hakuna promotions au bonus yoyote, na hata ikitokea kuna nafasi zimetangazwa ambazo ni za level ya juu yako, itakubidi uiombe kama mtu alie nje ya shirika na ufanye interview na asilimia kubwa wanazikosa hizo nafasi.
Mwisho wa siku unajikuta unaletewa supervisor na utamfundisha kazi. na lengo kuu la wao kufanya hivi ni kwasababu wanataka watu wapya kutoka nje ya shirika wasiojua mienendo ya shirika. na mara nyingi wale wasiokuwa na uvumilivu huwa wanaacha kazi baada ya muda mfupi wa kuajiriwa.
Serikali yetu imelala wakati vijana wao wananyanyaswa kwenye nchi yao na wageni. mashirika haya pia ya sheria au policy inayosema mzawa au national staff kwenye field level hawezi kufika level ya manager bali ataishia level ya supervisor kushuka chini.
Mpaka muda huu toka nimeanza kazi, kuna watu kama nane wameacha kazi au kufukuzwa kwa makosa ya kipumbavu.
Sasa naendelea kujiuliza kwanini nafasi za juu za mashirika haya bado zimeshikiliwa na foreigners ambao hata sheria za tanzania hawazijui? hauwezi ukaleta HR manager kutoka vietnam au mexico au kenya ambae hajui sheria za nchi au project coordinator kutoka kenya, pakistan au nigeria wakati wapo watanzania wenye sifa na vigezo zaidi ya hao wanaokuja kushika hizo nafasi.
Kwa mfano, wana tabia ya kutangaza nafasi lakini lengo kuu ni kucheza na sheria za nchi wakati wanajua kabisa wazawa watakaoomba hizo nafasi hakuna atakaepewa kwasababu wanataka kutengeneza hoja au mazingira kuwa hakuna mwenye vigezo ili walete watu wao wabaguzi kuja kushika hizo nafasi.
Mfano: HOM ni mkenya na DHOM alikuwa ni mkenya pia,lakini amemaliz muda wake ameondoka na nafasi wameitangaza lakini nina uhakika hiyo nafasi haitopata mtu na ataletwa raia wa kigeni kushika hiyo nafasi.
Kama kuna mhusika yoyote wa uhamiaji, wizara ya afya au serikali kuu ambae yumo humu tafadhali sana tunaomba muwachunguze hawa masharika kabla ya kuwaruhusu kufanya kazi ndani ya nchi yetu.
Vijana wa kitanzania wanateseka na kunyanyasika ndani ya nchi yao kwa kigezo tu cha kutokuwa na ajira.
Naomba kuwasilisha!
Mkereketwa Mzawa anaefanya kazi MSF