Masheikh 4, wameshinda kesi leo tarehe 4/6/2024 mahakama kuu Dar es Salaam

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
576
783
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

MASHEIKH 4, WAMESHINDA KESI LEO TAREHE 4/6/2024 MAHAKAMA KUU DAR ES SALAAM MBELE YA JAJI MHINA

POLISI WAMEWACHUKUA

“Kwanza kabisa tunamshukuru Mwenyezi Mungu na pili tunawashukuru sana Shura ya Maimamu”.

Hayo ni maneno ya Sheikh Zahaki Rashid mara tu alipotoka katika chumba cha Mahakama na kukumuona kiongozi wa Shura.

Sambamba na viongozi wa Shura walikuwapo mawakili 4, waliowatetea.

Masheikh walioshinda kesi leo ni:

1. Zahaki Rashid Ngai.
2. Chande Rashid Njawi.
3. Jihadi Gaibon Swaleh. Na
4. Rashid Omari Mnigwa.

Masheikh hawa walikamatwa na polisi mwaka 2015, na kufunguliwa mashtaka ya kufanya vitendo vya Ugaidi.

Hata hivyo kwa zaidi ya miaka 8, upande wa serikali walishindwa kuleta ushadi Mahakani.
Mwaka huu mwezi wa 4, ndipo shauri lilipoanza kuzungumzwa na leo Mahakama Kuu imetoa hukumu ya kuwaacha huru baada ya kutowaona na hatia yoyote.

Katika hali ya kushangaza mara tu baada ya kutoka katika chumba cha Mahakama, askari wa jeshi la polisi waliwachukua na kuondoka nao bila kuwataarifu wao na ndugu zao wanawakamata kwa kosa gani.

Shura ya Maimamu baada ya kufuatilia imegundua Masheikh hao wanashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam.

Masheikh hao wamekaa gerzani kwa miaka 9.

Shura inafuatilia kushikilwa kwao na itatoa taarifa ya kinachoendelea.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA OFISI YA KATIBU MKUU SHURA YA MAIMAMU TANZANIA.
 
Hao ni watuhumiwa, kwa sababu huko Magereza hawakwenda kuhubiri dini, usheikh wakiwa misikitini kwao.
 
Ni jambo jema, kinachonisikitisha ni watu wasio na hatia kusota gerezani kwa miaka kibao wakingojea haki yao. Ni jambo la fedheha.
 
Hapo wameachiwa, wakamatwe, wachomwe sindano za kufa za muda mrefu, waachiwe mtaani, wasubiri kiama.
 
...Na hukumu ni kwa uadilifu. Hakika, Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki." (Kurani 49:9)

Tunafaa hata kuwa waadilifu kwa wale tunaowachukia, kama vile Mungu anavyosema:

"...Wala kuchukia wengine kusiwafanye kuacha uadilifu. Kuweni Waadilifu; hivyo ndivyo kuwa karibu mno na uchaMungu...." (Kurani 5:8)

Mtume Muhammad alisema: "Enyi watu, jihadharini na dhuluma,[5] kwani udhalimu utakuwa giza siku ya Kiyama."[6]
 
Hapo wameachiwa, wakamatwe, wachomwe sindano za kufa za muda mrefu, waachiwe mtaani, wasubiri kiama.
Kama serikali ingekuwa legelege Tanzania kungekuwa na hali mbaya ya usalama,kwasababu hata mahubiri yao yamejaa chuki kwa wasio waislamu na ndio maana bin salmani kaanza kufuta na kupiga marufuku Hadith za chuki ambazo ndizo masheikh wamezikalili.
 
Kama serikali ingekuwa legelege Tanzania kungekuwa na hali mbaya ya usalama,kwasababu hata mahubiri yao yamejaa chuki kwa wasio waislamu na ndio maana bin salmani kaanza kufuta na kupiga marufuku Hadith za chuki ambazo ndizo masheikh wamezikalili.
Kabisa.
 
Naona wanataka kuua hoja ya kuuzwa Bahari na madini yetu. Hautuwaelewi. Tunataka mkataba mlioingia na hao wakorea
 
Back
Top Bottom