Mashahidi 9, vielelezo 10 kutumika katika kesi ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Raia Mwema

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,717
13,467
Mashahidi 9 na vielelezo 10 vitatumika katika kesi namba 407 ya 2022 ya kimtandao katika Kundi la WhatsApp inayokambili mwandishi wa habari za afya na uchunguzi wa Gazeti la Raia Mwema, Mary Victor na wenzake wawili, Asha Mahita na Rogers Simeo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Glory Nkwera amesema ushahidi huo unatarajiwa kuanza kutolewa Januari 17, 2023 kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.

Katika kesi hiyo Maria Victor anatuhumiwa na makosa matatu likiwemo la kutumia laini ya simu ambayo imesajiliwa kwa jina la mtu mwingine (Asha Mahita), kutuma taarifa ya uongo kuhusu maradhi ya UVIKO-19 katika Kundi la Waandishi kwenye mtandao wa WhatsApp.

Naye Asha Mahita na Rogers wanatuhumiwa kwa pamoja kushindwa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) juu ya mabadiliko ya umiliki wa laini hiyo ya simu yenye namba 0715166210.

Katika kesi hiyo, Mary na wenzake wanawakilishwa na wakili kutoka Taasisi ya Sibaba Alex Masaba na wakili kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Anti Human Traffic and legal Initiatives Frank Mposso.

Akizungumza na Raia Mwema mahakamani hapo mapema hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TATILI, Godfrey Mpandikizi alisema: “Tumeamua kuongeza nguvu ya kisheria tukishirikiana na wakili mwenzetu Alex Masaba kuhakikisha haki inatendeka.

“Mwandishi wa habari anapofanya wajibu wake kihabari hatakiwi kupata vitisho au misukosuko ya aina yoyote ile kwa sababu anatimiza moja ya jukumu lake, taasisi yetu kama mdau wa waandishi wa habari ina jukumu kubwa kumsaidia mwandishi wa habari au chombo chochote cha habari.

“Ndio maana taasisi yetu inatoa mchango wa hali na mali kisheria kuhakikisha mwandishi anakuwa salama na kuendelea kutimiza majukumu yake kama kawaida.”

Washtakiwa wote wamekana mashitaka na wapo nje kwa dhamana huku simu za baadhi ya washtakiwa, vitambulisho vyao ikiwemo simu ya mkurugenzi Mbaraka Islam zikiendelea kushikiliwa katika kituo cha polisi kati (Central).

Pia soma = Mahakama yawaachia huru Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Raia Mwema na wenzake wawili
 
Back
Top Bottom