Mashabiki wa Vipers SC tukutane hapa

mganda og

Senior Member
Feb 23, 2023
139
472
Uzi huu ni Kwa wale wapenzi na mashabik wai vigogo kutoka Uganda hapa nazungumzia Vipers Sports Club.
Klabu hii yenye maskani yake jijin Kampala ndio mabingwa wa ligi ya Uganda.

Siku ya jumaosi tunawakaribisha Simba kutoka nchini Tanzania mchezo utakaopigwa St Mary's Stadium-Kitende

Niwatoe hofu mashabiki na wapenzi wote wa Vipers tu kuwa Jumamosi huyo Simba atapigwa sio chini ya goli 5 na ataendelea kubuluza mkia wa kundi letu paka mwisho maana yeye ndio kibonde wankundi letu.

Na Kwa wale mashabiki wao ambao Wana mpango wa kusafili kuja huku Uganda kutazama pambano hili nawaomba iyo ela Yao bora wanywee bia maana kipigo tutakachompa Simba sio cha kawaida.

Karibuni sana kuipa shavu timu yetu hii ya vipers ili tuungane na Raja kusonga mbele hatua ya robo fainali.

Mungu ibariki Uganda, Mungu ibariki Afrika Mashariki
 
Niwatoe hofu mashabiki na wapenzi wote wa Vipers tu kuwa Jumamosi huyo Simba atapigwa sio chini ya goli 5 na ataendelea kubuluza mkia wa kundi letu paka mwisho maana yeye ndio kibonde wankundi letu.
Vipers silaha yao kubwa ni defence, ni wagumu kufungika (pamoja na kwamba walifungwa 5 na Raja, nazungumzia kwa ujumla). Lakini kwa upande wa kufunga mabao, sio wazuri kabisa, wanayatafuta mabao kwa tochi. Hali hii ni kote kote, kwenye CAF CL na kwenye ligi yao
 
Unachekesha wewe mtanzania, yaani km juzi tu mlikua mnataka kumsajili Mshambuliaji wetu manzoki? Kwaio magoli hayo aliyokuwa anafunga manzoki yalikuwa ni ya wapi? Au kumbe mlikua mnataka kusajili Mshambuliaji asiyefunga magoli??
 
Manzoki yupo China, sio Vipers. Tatizo unatafuta ligi ya ubishi. Nenda kaangalie mechi 20 za mwisho alizocheza Vipers halafu uangalie kama kuna mechi ngapi alizoondoka na goli 2. Hilo moja tu hawalipati kirahisi.
 
Back
Top Bottom