Mashabiki wa Simba Wengi humu JF wanaongoza kwa mihemko na Wameingia kwenye Mfumo wa mashabiki wa Utopolo

Ubaya Ubwela

JF-Expert Member
Jul 24, 2024
1,008
2,435
Mashabiki wa wenzangu wa Simba acheni Mihemko na lawama kwa viongozi zisizo na msingi kwa kuongozwa na mihemko na maneno ya mashabiki wa utopolo.

Kocha Fadlu Davis tokayupo Pre Season kule Misri baada ya game mbili za kirafiki alisema kuna tatizo kwenye safu ya Ushambuliaji na mchezaji anaeonekana hayupo kwenye mipango ya Kocha ni Fredy Michael Na si Mukwala kama wengi Mnavyoaminishwa na mashabiki wa Utopolo.


Tumpe kocha mda atengeneze timu kwa vile anavyoona yeye, hizi lawama kwa viongozi hazima maama yoyote Hitaji la kuongeza mshambuliaji ni takwa la kocha na si Viongozi na ni muhimu kocha Asikilizwe na kupewa mahitaji anayoyataka ili kufanikisha mipango yake, ili kama baadae atashindwa ambiwe tulikupa kila ulichokihitaji.

Ateba si Mchezaji Mbaya kama mnavyoaminishwa na takwimu za hivi karibuni, mchezaji kushindwa kufanya vizuri na timu fulani na kuhamia kwingine na kufanya vizuri si Jambo geni.Mashabiki wa Simba Mnapenda kulalamika sana na malalamuko yenu hayaba maana yoyote .
IMG-20240807-WA0001.jpg
 
Sasa mchezaji ameshindwa kufanya vizuri huko alipotoka anakuja Simba kufanya nini, majaribio????

Hovyo kabisa hii michezaji ya kuokota okota sijui huwa tunaisajili ya nini?
Baleke amekuj kufanya nini utopolo, maana ndiko mnakochukulia mifano ya ulinganisho?
 
Tatizo sugu ili ni la kuchukua wachezaji toka kwa mawakala bila kuangalia uwezo zaidi ya maslahi binafsi ya 10%
Hakuna mchezaji asiyemilikiwa na wakala, hawa akina Mavambo tumewatoa kwa mawakala hawa hawa, Na % kubwa hatukumjua mavambo kabla hajatua msimbazi

Kipa Camara alianza kupondwa na wana utopolo na wengi mkaingia mkenge sa hizi wameufyata acheni kocha apewe anachohitaji atengeneze timu, tumlaumu mwishoni
 
Sasa mchezaji ameshindwa kufanya vizuri huko alipotoka anakuja Simba kufanya nini, majaribio????

Hovyo kabisa hii michezaji ya kuokota okota sijui huwa tunaisajili ya nini?
Fredy alifanya vizuri huko alikotoka mbona hapa hajafanya vizuri. Torres alifanya vizuri alipokuwa na riverpool lkn alipoenda Chelsea alifanya nini?
 
Mashabik mihemuko wakiweza jizuia kufata propaganda za utopolo na kukaa na timu yao na kuivumilia ikiwemo kuvumilia wachezaji na kuwaamini timu itakuja kuwa balaa hii..
Ila wanapelekeshwa na upepo wa nje ndo kwanzaa mechi 2....
Inashangaza sana...
Ngoja tukae pembeni kwanza tuishabikie timu yetu huku mitaani maana humu JF kila mtu ni kocha...
 
Okrah Magic, aliposajiliwa na utopolona kucheza mechi mbili za mwanzo mashabiki upepo wa simba walianza kuutukana uongozi leo hii yuko wapi?


Acheni mihemko wazee ndo kwanza hata ligi hazijaanza.
IMG-20240813-WA0012.jpg
 
Watanzania wengi akili ya mpira hawana sasa wewe unataka kila siku timu yako ichukuwe kombe yaan iwe inafanya vizuri hicho kitu hakiwezekani wamesahau uti alikaa miaka bila ya kubeba kombe Leo hii uti anafanya wanashangaa hata Madrid barca man u Arsenal Brazil haziwezi kuwa vzr miaka yote muhimu ni kuvumiliana uti walikaa miaka minne bila ya kombe kweli binadamu tumeumbwa kusahau
 
Mukwala hakuna striker pale Ahoua naye anakimbiakimbia tu hovyo uwanjani Mutale ni saido aliyezubaa bora hata saido.Cha msingi Ong bak aondoke na Mo atuachie timu yetu
 
Batiki zipo madukani, anayeona kuwa chura ni raha awe chura tu ila asirudi, akirudi anakuwa Simba asiye na mkia.
 
Back
Top Bottom