Jina la beki wa kati wa
Real Madrid na nahodha wa timu hiyo
Sergio Ramos bado linazidi kugonga headlines katika mitandao ya kijamii,
Ramos bado amekuwa akijadiliwa na mashabiki wa soka kuhusiana na kadi yake nyekundu aliyooneshwa wakati wa mchezo wa
El Clasico dhidi ya
FC Barcelona.
Sergio Ramos alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 77 ya mchezo baada ya kumchezea faulo
Lionel Messi inayoaminika kuwa ni mbaya kwa mashabiki wa
Barcelona, licha ya kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja walitamani kuona
Ramos akikosa mchezo zaidi ya mmoja kwa kosa hilo.
Beki huyo kwa sasa ataukosa mchezo mmoja wa
Real Madrid wa siku ya Jumatano dhidi ya
Deportivo utakaochezwa katika uwanja wa
Municipal Riazor, kitendo ambacho hakijawafurahisha mashabiki wa
Barcelona na kulaumu mitandaoni wakiamini
Ramos anastahili kukosa mchezo zaidi mmoja kwa faulo aliyomchezea
Lionel Messi