Masekretari na mareceptionist maofisini ni vigingi kwa waomba kazi

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,376
29,736
Habari zenu!
Kama kichwa cha habari kinavyosema, ila sio kwa wote ila ni asilimia kadhaa, hawa ndugu zetu yaani masekretari na mareceptionist WANAWAKE wengi wana roho ya korosho kwa wale wanaopeleka barua za maombi ya kazi katika makampuni na maofisi.

Hawa wadada maana sio wamama, hupokea barua za hawa vijana wanaoenda omba kazi na kutoa maneno kuwa zimefika. Wengine kwa jinsi anavyokuongelesha tu utajua barua yako ndo imefika mwisho. Wafanyacho ni hawazipeleki kwa wahusika wenye kuzipitia na kufanya maamuzi. Eidha atairarua baada ya wewe kuondoka na kuiweka ktk dustbin au ataondoka nayo kwenda kwake na kuiangamiza huko.
Nasema haya sababu imewahi nitokea na baada ya kufuatilia kwa bosi muhusika ilidhibitika kuwa secretari hakufikisha barua.
Wiki ilopita imemtokea mwenzangu HIVYO naona ni katabia ka hovyo sana kwa hawa madada zetu.

Tafadharini, acheni KUWABANIA wenzenu, maisha ni kutafuta sio kubaniana, huwezi jua bahati ya mwenzio imelalia wapi.

BADILIKENI, ACHENI HIYO TABIA YA KURUDISHANA NYUMA.
 
Heri kutuma kwa posta kumbe hata kwa njia ya kawaida japo hakuna uhakika kama zinafika pia
 
Makampuni mengi wakiwa wanataka kuajiri huwa wana platform fulani za kuomba kazi kama kutangaza ajira, interview, shotlist, n.k
sasa wewe from nowhere utoke ulikotoka ulete mbahasha wako ofisini wakati utakuta kwa wakati huo ofisi haiitaji watu wa kuajiri sie mbahasha wako ma cv kama ripoti ya CAG ya nini sie.. tukiweka ofisini sijui stoo ndio mwanzo wa kuleta panya so njia sahihi ni kuyachomelea moto mbali

hahah sipo serious sana
 
Wewe ndio wale wale wenye roho za korosho, sema nakupa hongera kwa kuitambua roho mbaya yako, mana kuna wengine wana roho kama yako lakin wanajiona maraika mbele za watu. Haikuwa na haja ya ku-compensate eti sipo "serious sna" hiyo ndio roho yko
 
Wewe ndio wale wale wenye roho za korosho, sema nakupa hongera kwa kuitambua roho mbaya yako, mana kuna wengine wana roho kama yako lakin wanajiona maraika mbele za watu. Haikuwa na haja ya ku-compensate eti sipo "serious sna" hiyo ndio roho yko

tatizo lako ni kuwa mie naongea reality nikiwa emotionless.... wewe unaongelea unreality ukiwa na emotional breakdown
 
kiukweli wapo wanaozingua ila wengi wao hawawazuii kwa kuwakomoa ila wanatimiza majukumu yao..

ukiajiriwa ni kama umeolewa so receptionist haruhusiwi kumruhusu mtu yoyote kuingia ofisini bila approval.. ndio maana wana kuuliza unamuhitaji nani.. na then wanampigia simu kwanza..

na hata barua kama kaambiwa asipokee barua ovyo ovyo hawezi pokea..

ike kazi sio yake yeye anatimiza majukumu tu
 
Ila kuna watu wanapata kazi kwa mtindo huu, unapewa tip na mdau aliye ndani kuwa kuna nafasi, sio makampuni yote hutangaza, wafanyakazi wa ndani kwa ndani wanakuwa na taarifa wanaleta watu wao na kwa wewe unaesibiri matangazo inasubiri forever.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…