Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 1,124
- 2,194
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Hamad Masauni ameeleza kuwa falsafa ya maridhiano ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan zimejenga umoja wa kitaifa, mapenzi na undugu bila kujali tofauti za kiitikadi zilizopo nchini Tanzania.
Waziri Masauni amebainisha hayo leo Jumanne Aprili 22, 2025 wakati alipokuwa akifungua kongamano la miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika Jijini Dar es salaam, akisema mbali na mafanikio hayo, falsafa hiyo imekuwa daraja la kuimarisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
“Kupitia falsafa hii mambo mengi yamefanyika, tumeimarisha mfumo wa haki jinai, uhuru wa kujieleza, uhuru kwa vyama vya siasa kufanya kazi zao, mazungumzo na ushirikishwaji, mabadiliko ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa na sheria ya Tume ya Uchaguzi.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Mama Samia ana majina mengi je, tukimuita Mama mageuzi tutakuwa tumekosea?” alihoji Masauni.
Akizungumzia maadhimisho ya Muungano, Masauni amesema falsafa hiyo imeimarisha uhusiano wa pande mbili za muungano.
Amesema misingi ya muungano imejengwa juu ya undugu wa kihistoria kati ya Tanganyika na Zanzibar, jiografia ya mataifa hayo na utashi wa wazee waliouamini umoja, mshikamano, ushirikiano na upendo.