Karibu CRDB "the bank that listen"Fikiria umeacha kazi zako kwenda benki kutoa pesa kwa ajili ya kununua bidhaa za biashara yako.
Huko benki unakuta wateja zaidi ya 100 huku wakiongezeka kadri muda unavyosonga.
Pamoja na kufurika wateja, dirishani kuna wahudumu wawili tu madirisha mengine matatu yakiwa yamefungwa tangu saa nne asubuhi mpaka saa nane hii, benki hii ya tawi la Kenyatta road haina kiti wala fomu za kukaa wateja, ni shida tupu hasa kwa wazee na akina mama wasioweza kusimama kwa muda mrefu.
Hivi kweli benki hizi hazina uwezo wa kuweka benchi au viti kwa ajili ya kukaa wateja wake? Kibaya zaidi hata wale wanaojaribu kuketi nje kwenye msingi wa benki baada ya kuchoka kusimama ndani wanatimliwa ili mradi ni shida tupu.
Ebu NMB Kenyatta road ongezeni ubunifu, kwa nini mtu kuja kuchukua au kuweka pesa yake asimamishwe masaa manne bila huduma?
CRDB Tanga hali ni kama hiyoKaribu CRDB "the bank that listen"
Duh mpaka una historia...hahah poleNakumbuka mwaka fulani nilikuwa naumwa lakini nikalazimika kwenda bank (NMB) kuchukua hela. Nilivyofika pale nilikuta foleni ambayo hadi leo sijawahi kukutana nayo popote pale. Nilifika pale saa tatu asubuhi na hadi saa saba mchana nilikuwa niko kwenye foleni bila kumfikia teller. Kuondoka ili kurudi siku nyingine nikawa nashindwa kutokana na shida niliyokuwa nayo. Na wakati huo miguu ilishachoka kusimama. Ikabidi niwaage wateja wenzangu wa mbele na nyuma yangu kwamba niko pembeni kidogo nasubiri foleni isogee. Baada ya kutoka kwenye foleni nikaenda pembeni ukutani nikachuchumaa kwa sababu hakukuwa na mabenchi au viti. Bahati nzuri meneja wa tawi alipita na kunikuta nimechuchumaa na kuniuliza kulikoni. Nikamwambia nimekaa sana kwenye foleni kwa zaidi ya masaa manne na pia naumwa. Alichonifanya ni kunipeleka ofisini kwake nikakaa kwenye kiti na yeye akachukua cheque yangu na kunihudumia hadi nikaondoka. Ni siku ambayo sitakuja kuisahau. Kwa kweli NMB foleni zao uwa siyo za kitoto.
Umeacha kazi zako kwenda kutoa pesa kwa ajili ya kununua bidhaa za biashara yako. Sasa unachukia nini kama umeenda hapo kuvinjari? Maana hukuwa kazini.Fikiria umeacha kazi zako kwenda benki kutoa pesa kwa ajili ya kununua bidhaa za biashara yako.