Marufuku kumwita mtu fulani: "Mwamba"

Setfree

JF-Expert Member
Dec 25, 2024
2,807
3,850
Imezuka tabia, siku hizi, watu wanapomuona mtu fulani ana msimamo thabiti, imara, wanamwita “Mwamba.”

Kwa mujibu wa Maandiko, "Mwamba" ni jina lenye uzito mkubwa kiroho. Jina hilo ni la Yesu Kristo peke yake, kama Maandiko yanenavyo katika 1 Wakorintho 10:4b.

Kumwita mwanadamu “Mwamba” ni kumpa utukufu asiostahili.

Yesu tu ndiye anayestahili kuitwa Mwamba.

Nawasihi kwa heshima zote, tusiguse utukufu wa Yesu.
 
Amen
Ni kweli mazoea yanetuharibu
 
Nilikuwa na boss wangu wa kike ,siku moja aliniamulia japo nahisi alikuwa kwenye mtanziko wa kifamilia maana alikuwa na hasira sana asubuhi ile basi alinikandamiza mbele ya seniors na majunior wote kwa maneno mengi mno .

Bahati jana yake sikulewa hivyo sikuwa hata na ujasiri wa kujibizana wala confidence ya kupinga alichokuwa anasema zaidi nikawa namuangalia .

Ila pasina kujitambua baada ya saa moja la kuchambwa na kugalagazwa kwa maneno magumu nilijikuta sina tena chembe ya heshima wala uoga nilimjibu vibaya mno na mwisho nikamwambia uwa ananipenda ila anashindwa kusema .

Maneno yale niliyamka mbele ya pannel ya taasisi yetu hakika watumishi wote wakubwa na wadogo wote walikiwepo ilikuwa siku ya huzuni kwa mama yule maana hakutaraji kama ningeweza kufanya vile .

Baada ya kikao mama yule aliniita ofisini kwake na rasmi akaniomba msamaha ila kubwa akasema mimi ni mwanaye hawezi kutamani kuwa na mimi hivyo nisiwe na hisia hizo ila zaidi akadai nifanye yaliyopita yamepita tufanye kazi na nisirudie kukasirika kiasi kile .

Ni mama mtu mzima ambaye ni rafiki yangu ,sana kwasasa .

Ila katika viunga vya ofisi zetu kila nilipokatisha jina mwamba limetamalaki sana mpaka leo .

Hivyo natamani unishauri nifanyeje waache mara moja kuniita jina kubwa nisilostahili mchungaji Setfree
 
Ujinga mwingine ni huu Yan Bora ungekaa kukemea hawa wanaojiita manabii na mitume feki wanadanganya watu mchana kweupe
Soma huu uzi
 
Imezuka tabia, siku hizi, watu wanapomuona mtu fulani ana msimamo thabiti, imara, wanamwita “Mwamba.”

Kwa mujibu wa Maandiko, "Mwamba" ni jina lenye uzito mkubwa kiroho. Jina hilo ni la Yesu Kristo peke yake, kama Maandiko yanenavyo katika 1 Wakorintho 10:4b.

Kumwita mwanadamu “Mwamba” ni kumpa utukufu asiostahili.

Yesu tu ndiye anayestahili kuitwa Mwamba.

Nawasihi kwa heshima zote, tusiguse utukufu wa Yesu.
Kwa nini unanunua sonona-nene kwa bei rahisi hivyo?Kuna watu wanaitwa Jesus,God,Emmanuel,Raphael na makadhalika mengi tu.Je,unajua maana ya hayo majina kabla ya hilo la Mwamba?
 
Imezuka tabia, siku hizi, watu wanapomuona mtu fulani ana msimamo thabiti, imara, wanamwita “Mwamba.”

Kwa mujibu wa Maandiko, "Mwamba" ni jina lenye uzito mkubwa kiroho. Jina hilo ni la Yesu Kristo peke yake, kama Maandiko yanenavyo katika 1 Wakorintho 10:4b.

Kumwita mwanadamu “Mwamba” ni kumpa utukufu asiostahili.

Yesu tu ndiye anayestahili kuitwa Mwamba.

Nawasihi kwa heshima zote, tusiguse utukufu wa Yesu.
Mkuu angalia biblia ukiichunguza sana kuna hekima na maarifa unaweza kuvipoteza katika Jamii inayokuzunguka, wanaume kila tunapokutana haijarishi tunajuana au hatujuani huwa tunapenda kutiana moyo kupitia kuitanana majina ya kishujaa mfano "MAN" " MWAMBA" "BRO" n.k, lakini pia Kuna watu wanaitwa Angel, Godfrey Kwa kifupi God n.k, haimaanishi wakiitwa hivyo wanachukua utukufu wa vitu/viumbe kupitia majina, wanawake huwa wana majina yao "SHOGA YANGU" "SHOST" n.k kulingana na mahali waliookitana na walivyozoeana ujumbe wako unaweza kuwa na mantiki kwa walengwa ila jitahidi kucontrol "Roho mtakatifu" na "mihemko" kila utakapotaka kuwasilisha ujumbe unaomgusa Mwenyezi Mungu
 
Imezuka tabia, siku hizi, watu wanapomuona mtu fulani ana msimamo thabiti, imara, wanamwita “Mwamba.”

Kwa mujibu wa Maandiko, "Mwamba" ni jina lenye uzito mkubwa kiroho. Jina hilo ni la Yesu Kristo peke yake, kama Maandiko yanenavyo katika 1 Wakorintho 10:4b.

Kumwita mwanadamu “Mwamba” ni kumpa utukufu asiostahili.

Yesu tu ndiye anayestahili kuitwa Mwamba.

Nawasihi kwa heshima zote, tusiguse utukufu wa Yesu.
secretarybird ni mwamba kweli kweli.

Cc: Nomadix holoholo nyau de adriz
 
Back
Top Bottom